Sunday, June 29, 2014

KWA WALE WENYE NYUMBA ZA GHOROFA.....



 Hii imekaaje.....unaonaje.......je unaweza uka iweka kwenye ngazi zako hapo nyumbani. ....

RANGI ZA NJE ZA NYUMBA........ZINAPATIKANA KWENYE RANGI ZA DULUX PIA.....

 Ukiangalia nyumba hizi....sio tuu kwakua ziko nje ya nchi kwa wenzetu.....lakini pia zinavutia...na zinapendeza....kuanzia juu kwenye bati..mpaka chini...na garden pia...yaani unaanza kukaribishwa na mazingira na nyumba pia kabla ya mwenyeji...
 Uzuri wa nyumba hizi....ni mpangilio mzuri wa ujenzi...rangi na garden. ...ila ntaongelea rangi leo....tumekua tukidharau rangi jamani...ama kutokujua....

 Hua ninasema kila mara kua....kabla ya kupaka rangi. ..ukuta unatakiwa kutayarishwa vizuri....bila kuruka stages.....nani mwiko kutumia gypsum powder.....iwe ni ndani ama nje....products za skimming ziko.....kuna smooth over ya dulux ama stuko ya sadolin....ni wewe tuu na uwezo wako...
 Sijui kama hiliswali hua mnajiuliza wapendwa.....hivi kweli...hua mnawekaga budget ya rangi...kwenye nyumba zenu....ama ikifikia kwenye rangi ndio kukurupuka....na ndio maana nyumba zinalipuliwa.....mtu umejenga nyumba ya mfano ninachukulia....gharama ya nyumba ni 50 million. ..haya ukija kwenye skimming na  rangi ndani na nje unataka kutumia laki 8....kweli jamani....si ndio baada ya miezi 3 kama sio 6 rangi inabanduka...ama kupauka...
 Unajisikiaje kuangalia nyumba hizi zilivyo na Finnishing nzuri na si zinavutia sana....sasa wenzetu wana invest...kwa muda mrefu..na aiku zote rahisi gharama....nyumba ni yako bado unaifanyia ubahili....nani sasa aje kukufanyia kazi nzuri.....kila ukiambiwa unaangalia bei badala ya kazi na products zitakazotumika kwenye nyumba yako...
 Naomba niwaambie kitu wadau.....kua in worldwide. .....Finnishing ya nyumba ni gharama mno.....tena mno.....ila huku watu tunajua kua kujenga ndio gharama na Finnishing ni rahisi...halafu nyumba hiyo hiuo utakuta....furniture zilizowekwa ni za mamilioni.......sasa najiulizaga....hivi kweli hapa...Finnishing hairidhishi....unadhani hizo furniture zitaonekana kweli....na umekwepa nini sasa......
 Haiingii akilini unajibahilia kwenye Finnishing ya nyumba yako kweli....hivi unajua kua unatakiwa kuishi vizuri kadri uwesavyo....especially. ..sehemu ya kulala...maana ndio 80%ya maisha yako yanategemea upumzike vizuri.....
Kama ulivyojipanga kwenye ujenzi...na Finnishing jipange hivyo hivyo.....narudia tena...Finnishing ni gharama kuliko ujenzi...na products za dulux ndio zimekuja kumaliza utata huo......

Ukituita homez deco....hatulipui kazi wala kuruka stage...na tunafanya kazi ya uhakika...sasa uamuzi unao wewe....kujenga nyumba nzuri..then umalizie na Finnishing isiyokua na ubora...then uweke furniture za gharama.....

Friday, June 20, 2014

UNA NGUO UNAZOZIPENDA SANAAA................



 Hivi unajua kua unaweza ukawa na nguo zako unazozipenda...halafu zile rangi za nguo hizo ukazi apply nyumbani kwako.....kwenye chumba chochote kile.....



Kucheza na rangi ni kazi na inahitaji muda na utulivu ili uweze kupata kile unachokihitaji katika nyumba yako.......sasa basi hii ni mojawapo ya wazo la kukusaidia katika uchaguzi wa rangi......

Hizi ni baadhi ya nguo na rangi zake.......najua wewe unazo nguo unazozipenda......basi sawa...haya zifanyie kazi........


Tunapatika pia instagram @homezdeco


KORIDO ZETU.......




Ni wazo tuu.....kwenye korido za nyumba zetu.....mimi kwa mpaka sasa katika kazi yangu hii...wengi wetu tunajenga nyumba zikiwa na korido ndogo..kiasi kwamba huwezi kuiwekea decorations yoyote ile......

Swali ni kwamba viwanja vyetu ni vidogo....ama ni tunavyochorewa ramani hatutilii maanani ama tatizo ni nini?......

Tusaidiane katika hili.....

RANGI YA PINK......BAFUNI.....




Umeshawahi kufikiria kua.....rangi hii inaweza kukaa bafuni.....maana tumezoea sana rangi hii iwepo tuu kwenye vyumba vya watoto....wetu wa kike...

Mara nyingi rangi ya pink inaendana na rangi ya papo......hilo nadhani linajulikana....

Halafu jamani......inawezekana kwenye mabafu yetu tukawa tunaweka tiles half.....ukutani....ili eneo linalobaki tukapaka rangi.....na hii itakusaidia kila mara unabadilisha rangi na kufanya bafu/toilet kua na muonekano mzuri na kubadilika mara kwa mara.....tiles tunazoweka zinatu limit mno....na hatimae tunachoka haraka.......


Endelea kua nasi kwenye instragram yetu @homezdeco

EMAIL: homezdeco@yahoo.com TEL: 0713 - 920565


Wapendwa wadau....naomba maulizo ya bei tutumie njia ya email ama simu....kutokana na sababu zilizo nje ya uwezo wetu..

Nawashukuru sana,.....na samahani kwa usumbufu.

Thursday, June 19, 2014

DECORATIONS ZA UKUTANI. ......ZINAPATIKANA HOMEZ DECO. .....

 Karibu homez deco......decorations hizi unaweza kuweka kwenye ukuta wa tv ukuta wa kwenye sofas,  ama dinning ama chumbani. Na hata korido...na zikapendeza mno...

 Zinapatikana katika rangi yoyote ile....na kwa size yoyote ile...tumezoea picha tuu lakini hata hizi decorations zikapendeza mno ukiziweka...

Kwa maelezo zaidi naomba tuwasiliane kwa simu 0713 920565 ama email homezdeco@yahoo.com.

KWA MFANO ...UNAONAJE MOJAWAPO KATI YA HIZI IKAWA NI MASTER BEDROOM YAKO......



Kuna msemo usemao .....kupanga kuchagua.........Hivi unajua ukiamua unaweza kua na masterbedroom nzuri tuu jamani....maana hakuna cha ajabu hapo......kila kitu kinajionyesha.....

 Niwewe tuu kuamua kua nataka kulala sehemu nzuri na safi...nayakuvutia....na asikudanyanye mtu....sehemu yako ya kulala ikiwa nzuri..hata kazi unaweza kufanya kwa juhudi na kwa ufanisi......mwili unatakiwa kupumzika sehemu safi na nzuri....na sio eti mpaka uwe na chumba kikubwa..ama ndio misemo yetu ...tunasubiria kua na nyumba zetu...ndio tulale pazuri jamani.....sasa kwa mfano ndio haujabahatika.....inakuaje...uendelee kukaa mahali...ndivyo hivo hivo tuu.......

Muonekano wako nje uendane na muonekano wako wa ndani ya nyumba yako jamani.....vaa yako nayo iendane basi naya ndani kwako basi......inawezekana ukiamua...na sio eti mpaka ukajifilisi.....ni kujipanga tuu...na kuamua.....


Wednesday, June 18, 2014

BRONCH.........PINI ZA KWENYE NGUO......UREMBO WA NGUO...WAWEZA PATA RANGI YA NYUMBANI KWAKO........


 Wengi wetu hizi pini hizi tunazo.....na tunazitumia kufungia nguo zetu.....kama suti...ama blouse...etc...na huongeza mvuto zaidi..kwenye nguo zetu.....

Lakini sasa unaweza kupata rangi za kupaka katika nyumba yako kwa kupitia pini hizi....haswa katika ile pini uipendayo sana....unaweza kuweka rangi hizo sebuleni kwako...chumbani ama korido etc.......na kukavutia mno


 Hizi ni baadhi ya pini hizo....na rangi zinazoendana.....na zilizokuwepo katika pini hizi.....ukiwa makini utapata rangi uzipendazo......
 Hebu niambie ni group gani umelipenda na ungependa nikusaidie vipi.....katika uchaguzi huo.....na tukakuuzia rangi zetu za Dulux ama Sadolin kwa bei nzuri kama rangi zenyewe...na ushauri pia utapata...ili kuweza kupendezesha nyumba yako.....

Ukiwa na nyumba nzuri...na yakuvutia......utakua na amani ya moyo na furaha muda wote......

Kupanga  kuchagua....furnitures zako nzuri za gharama haziwezi kuonekana kama rangi ya nyumba haivutii.......uamuzi unao wewe.....

Tuwasiliane namba 0713 - 920565, ama email: homezdeco@yahoo.com

PUNGUZO LA BEI KWENYE VITANDA VYA CHUMA......AINA YOYOTE ILE........10% OFF.......WAHI SASA TOA ODA YAKO ......


Tunapenda kuwajulisha wateja wetu wote kua Homez Deco inatoa punguzo la bei la asilimia 10 katika bidhaa zake za vitanda vya chuma...karibu utoe oda.....

Wasiliana nasi kwa namba 0713 - 920565, ama email: homezdeco@yahoo.com


Bei Tshs 380,000. size 5 by 6

 Bei Tshs 380,000. size 5 by 6
 Bei Tshs 380,000. size 5 by 6



Bei Tshs 450,000. size 5 by 6




OFA HII ITADUMU KWA MUDA WA MWEZI 1 TUU.........WAHI SASA........HUJACHELEWA...

Tuesday, June 17, 2014

RANGI ZA SADOLIN......ZINAPATIKANA HOMEZ DECO........


Tunapenda kuwajulisha kua sasa utajipatia rangi za Sadolin kwenye ofisi zetu za Homez Deco....

Kampuni ya Sadolin ndio iko pia na rangi za Dulux.......

Tunaendelea kuwarahisishia kwenye upande wa rangi.....kama tunavyojua rangi za Sadolin ni nzuri... na ziko katika ubora unaotakiwa...

kuna Wash n Ware, ama Silk..zote ni aina moja ila tuu majina......kuna Weather guard, Emulsion rangi za maji.  etc....

Tuna lita 4 na lita 20


Wasiliana nasi kwa email: homezdeco@yahoo.com   au  tel: 0713 - 920565.

RANGI ZA DULUX ZIMESHUKA BEI...............TUWASILIANE KWA NAMBA 0713 - 920565 AMA EMAIL: homezdeco@yahoo.com

Tunapenda kuwafahamisha wadau wote kua sasa rangi za dulux zimeshuka bei kwa kiwango kikubwa mno....na hii ni kutokana na kwamba tunapenda wadau wote waweze kupata rangi hizi na kuweza kupendezesha nyumba zao..

Naomba ifahamike kua dulux sio tuu ni rangi za ukuta ni SOLUTION... ya ukuta....kuanzia skimming, kwenye matayarisho ya ukuta.....na pia kuna products nyingi za nyumba nzima kwenye suala zima la finnishing ya nyumba yako ama ofisi...

Dulux kuna rangi za ndani na za nje, kuna vannish kwa ajili ya mbao,  kuna skimming plaster ambayo imeshachanganywa kabisa kumrahisishia fundi....kuna za grills...hammirates....etc

Ninachoweza kusema ni kwamba jamani nyumba ni finnishing pia ,...maana tumekuwa tukikazana sana kwenye ujenzi kusimamisha nyumba... ila inapokuja suala zima la finnishing...tumekua ni waoga wa bei......ila nyumba ukiangalia kwa kweli ni ya gharama....sasa ....ila hili ntakuja kulizungumzia siku yake ingine.....


 Dulux paints inatumika kokote kule.....majumbani, ofisini, nyumba za kuabudu....etc....

 Hii ndio color chart yetu ambayo ina shades...zaidi ya 3200. yaani hapa huwezi kukosa rangi unayoitaka....iwe dark or light.....na pia uzuri wa dulux....hizi rangi ukishatoa order ni kua huwezi kuichakachua....unachokitaka ndio utakachokipata.....sio mara fundi anaongeza rangi nyeupe ama tonner....hapana...na inaokoa muda wa mafundi kuitumia....na ni rahisi kuitumia......ntaleta somo lake kuhusu hili..
 hii ni product ya skimming inatumika ndani na nje......na ni rahisi kuitumia maana imeshachanganywa.....jamani gypsum powder ukutani ni sumu ya rangi......

 ni kweli dulux uta save hela yako. lita 1 ya dulux inapaka square meter 10 kwa mpako 1 wa kwanza....na inawahi kufunga ukutani......
 Product hii ni kwa wale nyumba zinazosumbuliwa na ukungu....unyevu unyevu......kwenye ukuta....mpaka unakuta rangi haikai...ama kudumu.......kuna lita 1 na lita 5
 kuna somo linakuja kuhusu hii picha.........
 Hii hapa ni rangi ya grills ......kwenye grills....ni lazima upake vyote 3 ila kila unapopaka ni lazima uipe muda ikauke ndio upake,,,,,lakini sasa hii imechanganywa yote 3 na unapaka kwa maramoja.....na wale wanaokaa ukanda wa chumvi chumvi......chuma hulika....itawafaa sana hiii........

 Rangi za nje.......zipo pia.......na zina muonekano mzuri...na zinahimili joto, mvua na hali yahewa yoyote ile.....zinapatikana kwa lita 1 na lita 5
 Vannish pia ziko......aina tofauti tofauti.. inapatikana kwa lita 5
Silk ama wash n ware....pia zinapatikana.....inapatikana kwa lita 1 na lita 5

Monday, June 9, 2014

MABADILIKO YA EMAIL......

Napenda kuwajulisha..wote kua...kuanzia sasa...ile email ya sylvianamoyo@yahoo.com. ...haitotumika...tena...badala yake...tutatumia email:  homezdeco@yahoo.com.

Mabadiliko haya...yatasaidia...kujibiwa email kwa uharaka zaidi......

Na pia naomba maulizo yote ya bei....yatumwe humu kwenye hii email mpya...maana mtu uki comment kuuliza bei kwenye post zanyuma...inaniwia vigumu...kuanza kuitafuta post na kuijibu...na pengine nikijibu....unaweza usiione kwa urahisi....nankuona kama sijibu...

Ninajitahidi kurahisisha....vitu...ili twende sawa....

Asanteni sana.....na naendelea kuwakaribisha Homez deco...kwa mahitaji yako.....ya home decor....

HOMEZ DECO FLYER.....AND BUSINESS CARD........


Wadau wa homez deco.....napenda kuwajulisha kua...huu ndio muonekano wa fyler na businesses card...yetu..homez deco...itakavyoonekana...na kuanza kusambazwa.....katika maeneo mbali mbali....ya ndani na nje ya mkoa wa Dar -es- Salaam....

Nawashukuru sana wote...maana bila nyinyi wadau na wateja wangu...mie sio kitu....

Na hizo kwenye flyer ndio kazi tunazozifanya.....

Karibuni na endeleeni kua nasi....maana bado kuna mambo mazuri naendelea kuwaandalia...

Tuesday, June 3, 2014

IMEKUPENDEZEA..........COFFEE TABLE......






Umeionaje hii design ya coffee table.....imekuvutia.....

MAHITAJI YA GRILLS ZA MILANGO NA MADIRISHA......




 Tumepata mdau mwenzetu...yeye ana deal na kutengeneza grills. ...hizi zinazoonekana......

Homez deco tunapenda kumleta kwenu....mdau huyu na kazi yake hii.....





 Kwa mahitaji ya grills. ...wasiliana nae.kwa namba ....0717- 060 776.