Thursday, October 10, 2013

KABATI ZA JIKONI KATIKA MUONEKANO WA 3D

Katika muendelezo wa ku design 3d upande wa jikoni.



Naomba niwafahamishe wadau wote kua, kabla ya kufanya design ni lazima tujue kua jiko hili litatumikaje? na eneo letu litatutosha?  kuna aina mbili hapa, kuna jiko ambalo tayari limesha jengwa, na kuna lingine ambalo bado halijajengwa.

Kwa hili ambalo limejengwa tunachokifanya ni kucheza na space iliyoko katika ku design........

Ambalo halijajengwa tutaanza maandalizi, na kidogo hii hua nirahisi zaidi, ambapo tunahitajika kujua ni watu wangapi watahitajika kuwepo katika jiko letu, na je watapishana vizuri, na je nafasi itahitajika kiasi gani kwa ajili ya makabati, jiko, sink, fridge etc....

Nakumbuka kipindi cha nyuma nilishawahi kuzungumzia aina za majiko, na utachagua jiko lako liweje kulingana na ukubwa wa eneo lako la kiwanja. na hata kama limesha jengwa basi itaaangaliwa ni design gani inaweza kufaa kwa jiko lako, na kama kutakua na marekebisho madogo madogo basi yatafanyika ili kuweza kuwekwa sawa.




Kuna ile tabia ya kulazimisha kuweka vitu vikubwa wakati jiko lako ni dogo. ama vitu vidogo wakati jiko kubwa. vitu viwekwe kulingana na eneo.  Ninaongelea utakuta jiko dogo lakini mtu kaweka double door fridge.....ama jiko la plate 6, ama double sink....haya ni makosa...


Napenda kusema kua kabla ya kuanza ujenzi, jitahidi ujue kila sehemu itatumikaje, na kwa ukubwa gani.....watu wa design watakusaidia katika kuchanganua ama umwambie nini unataka hata kama ni vingi, halafu vitachambuliwa na kufanyiwa kazi.

Aina za jiko ni:
L-shape
U-shape
Gallery -shape
Straight line- shape
(nitarudia tena somo hili la aina za jiko)

Siku hizi naona baadhi ya nyumba tiles zinawekwa mpaka juu. napenda kuwaambia kua sio lazima, unaweza kuweka tiles katikati ya makabati ya juu na chini  na kukapendeza mno. sehemu inayobaki ikapigwa rangi.
Kwa kwenye ku fanya fittings za makabati, utakuta nyumba nyingi tunaacha nafasi kubwa kutoka kwenye cyling mpaka kabati inapoanzia.  Hilo ni kosa....maana ile nafasi inaweza kutumika. yaani hizo kabati zinakuwa ni ndefu, halafu kule juu unaweza kuweka vyombo vyako, vitu vyako aambavyo huvitumii, na vinakaa kiusafi maana vinakaa ndani ya makabati, na sio kukaa juu na kuonekana mlundikano wa mavyombo etc...

Sasa basi unaweza kuweka milango ya kabati ikiwa ni mbao mwanzo mwisho, ama milango inakwa na vioo.....uzuri wa kua na vioo kwenye milango, ni kua hautohangaiika kutafuta chombo unachohitaji, maana utakua unakiona kabla haujafungua kabati. na utakua unavipanga mara kwa mara maana utakua unaona kama vimevurugika katika upangaji wake.  na siku hizi unaweza kuweka taa kwa ndani kuweza kuona vizuri, na kuleta muonekano mzuri katika makabati haya.

Kwa upande wa madirisha ya jikoni. yasishuke chini sana ama kua juu sana. maana sink mara nyingi hukaachini ya dirisha, kwa kua outlets zake hutoka nje......na sink nalo sisikae juu sana mtu mpaka kuosha vyombo inakua ni vigumu.

Finnishing nayo inahusu sana hapa....je milango iweje ya kabati, vanish, sakafu, madirisha yaweje, pazia etc.....je utatumia mbao ama makabati ambayo ni ready made....yote hii ni kulingana na mfuko wa mteja.

Kila kitu kinakwenda kwa vipimo katika nyumba........hakuna kitu kinaitwa kukosea.....ni bora ujenziukafanyika taratibu kwa umakini na ufasaha, kuliko haraka haraka, ndio tunakoanza kulipua kazi.......naa hii ni kwa mteja na mfanyaji kazi....wote mnategemeana.


Vyombo hivi pia vinapangwa, na kwa rangi, ili kuonekana mpangilio wake na kuvutia.

Ni vizuri kufanya hii project kwa uhakika na pasipo haraka sana...ili upate kitu kizuri, na tuwe wasikivu wa wataalam wetu wanavyotushauri. bila hivyo utakuwa unapoteza hela kwa kuto kusikiliza ushauri wa kuweka vitu vinavyodumu katika jiko lako....

Katibu kwa huduma hii hapa Homez Deco.


Wednesday, October 9, 2013

MORE 3D DESIGN,

Tunaendelea ku design kwa 3d kwa wateja wetu........na hii husaidia kujua fanicha zikaeje, rangi ziweje, floor pia iweje,  mapazia ya rangi gani etc......



Karibu Homez Deco tuweze kukufanyia 3d Design hata kama umeshajenga na kuhamia, tunakukaribisha na tutakufanyia designing ya nyumba yako, ofisi, garden etc....

Wasiliana nasi......0713 - 920565 ama email: sylvianamoyo@yahoo.com

NB:
Hata kama unakaa nyumba ya kupanga, ama chumba kimoja ama viwili ama nyumba nzima......designing ni kwa watu wote.......

kukaa mahala safi, na penye mpangilio na salama ni muhimu kwetu sote.....

DAY BED....AVAILABLE BY ORDER @ HOMEZ DECO....(hardwood mkongo & mninga)

 Day bed hutumika kwa kupumzikia, unaweza kukiweka sitting room, balcony, ama kwenye korido kama ina nafasi......

 Homez Deco tunakuletea product mpya hii inayotengenezwa hapa hapa Tanzania....na mafundi wa Homez Deco, na ina finnishing nzuri kama unavyoona... rangi zozote utakazozichagua utapata kwa ajili ya mito yako.
Tunaweza kukuweka mbao kwa nyuma ya kiti ili mito ikae vizuri bila kuegamia ukuta, ama ikawa kama inavyoonekana......mito pia inapatikana Homez Deco.....

Karibuni sana kwa mahitaji ya Day bed........

Wasiliana nasi kwa mahitaji.......

Thursday, October 3, 2013

3D DESIGNS......



3d ni michoro ambayo huchorwa kwa kutumia computer na software maalum, ili kuweza kuona ni jinsi gani jengo lako itakua tayari baada ya kujengwa, na muonekano wake kwa ujumla, mpangilio wa fanicha ndani, na kuweza kukuonyesha makosa madogo na makubwa......

Hapa chini ni baadhi ya michoro ya 3d, ambapo tumeweza kuonyesha mfano wa nyumba itakavyoonekana baada ya kwisha kujengwa kwa nje....

3d yaweza kua niya garden, ya nyumba nje, ya mpangilio ndani, etc....ni wewe mwenyewe unahitaji nini.....


 Katika kazi yangu hii nimekua nikikutana na makosa mbali mbali ambayo wateja wangu wamekua wakiyalalamikia, kwamba jiko limekua ni dogo, ama chumba kidogo. ama hakutaka muelekeo huo.....mara vipimo havieleweki, rangi sio nzuri.......mpangilio wa fanicha. vitu haviendani. switch za umeme hazikuaa sehemu husika...etc.....ni tatizo kwa kweli......

Kitu kingine nimegundua kua katika ujenzi wa nyumba zetu, hua hatuna ule utaratibu wa kua wawazi kwa archtects(wachora ramani). Hausemi nini unataka, yaani we umeona nyumba ya flan basi unataka kua kama na yake na inabadilishwa kidogo tuuuu.......(copy and paste).

Jamni designs za nyumba ziko nyingi mno.....na ndio maana utakuta hapa kwetu nyumba zinafanana mno.......ukiona nyumba imebadilika basi ujue hiyo nyumba mwenye hakai sana hapa, kaja na mchoro wake toka nje.....

(nitalizungumzia hili siku ingine kwenye mada yake) inafika kipindi tuambizane ukweli....sasa......(let's be creative)

 kwa upande wa 3d, kama tungekua tunafuatilia ama kujua mapema, wengi wetu tusingekumbana na matatizo haya....maana saa ingine utakuta ukuta umezidi, inabidi kubomoa.......sasa hizo ni gharama zisizokua na maana.......

 3d inakusaidia kukuonyesha ni jinsi gani nyumba yako itakavyokua imekwisha na kwa muonekano gani....na sio tuu kwa nje, hata kwa ndani ya nyumba yako ama ofisi yako, utumie rangi gani, fanicha za aina gani, zikaeje, mapambo pia yaweje na yakaaje......

kwa mpango huu yaani haya makosa hayatakuwepo kabisaaaa
 Kuna wengine utakuta kiwanja ni kidogo nyumba ni kubwa....na hii hutokana na kwamba wengi wetu hatujui vipimo vinavyoandikwa kwenye ramani.......so ukiona tuu vile vipimo unajua nyumba ni ya kawaida,,,,,ama kiwanja kikubwa nyumba ni ndogo.......ama nyumba imekaa pembeni ya kiwanja, ama mbele unaacha nafasi kubwa nyuma, ama nyumba imegeuka.........wengine wananiambia unajua nyumba ya kwanza lazima kunakua na mapungufu, so tunajifunza kupitia hii ya kwanza.....itakayofuata tutakua tumeshajifunza....

Jamani, hakuna kitu kama hicho, ukitumia mtaalaam, tena mwenye kupenda kazi yake, kwa moyo wake wote na asiye na tamaaa.........Maana katika ku design 3d, jamani, kwanza akili iwe imetulia, na inahitaji muda wa kutosha, hakuna kitu kinaitwa haraka haraka.....kumbuka unatumia hela kujenga, na ukijenga umejenga......mambo ya kubomoa haifai na haipendezi..........
Yote haya niliyoyataja, ndugu wadau wangu ninakutana nayo mnooooooo, na ukiuliza kwanini imekua hivi, jibu ninalolipata ni kua wengi hawajui vipimo, na hawachorewi 3d kuona nyumba inakuaje ikishamalizika........


Homez Deco, tunapenda kuwakaribisha wadau, wateja, marafiki, ndugu, na wote, kua tumeanzisha huduma ya kuchorewa 3d.....na hii itakusaidia sana kuepuka gharama zisizohitajika wakati utakapoanza ujenzi wa nyumba yako ama ofisi yako........

Tutaendelea kuwaletea na kuwaelimisha kuhusu 3d designs, na nawaomba msisite kutupigia simu: 0713 - 920565 ama kutuandikia email: sylvianamoyo@yahoo.com


Tuesday, October 1, 2013

MAANDALIZI YA MWISHO WA MWAKA KATIKA NYUMBA ZETU.......

Wengi wetu tumekua na kawaida ya kujiandaa kwa ajili ya mwisho wa mwaka, kama kwenye maofisi basi tunapamba ofisi zetu kwa mapambo, na kama ni kwenye nyumba zetu basi nako tunajiandaa kufanya maandalizi.

Asilimia kubwa kati yetu ni kua hua katika kipindi hiki hua tunajitahidi kumalizia nyumba tunazojenga ili tunahamia, na wengine tunahamia kwenye nyumba zengine za kupanga....kubadilisha mazingira....etc.

Katika yote haya maandalizi yanahitajika.......na inategemea pia na nyumba yenyewe inahitaji nini.....

Kwenye upande wa matengenezo, ama rangi, etc....

Bila kusahau pia fanicha, nazo pia inatubidi tuangalie, kama zinahitaji marekebisho, ama zinahitaji kubadilishwa kabisaaa.....yote haya yanaanzia kwako na wewe mwenyewe.

Katika kipindi hiki cha mwisho wa mwaka ndio wengi wetu tanaangalia je yale malengo yetu tuliyoyapanga kwa mwaka mzima yamefanikiwa, ama yalikaribia kufanikiwa.

Napenda kukumbushia kua hiki ndio kipindi cha kufanya maandalizi ya nyumba zetu......kwa usafi, kutoa vitu ambavyo hauvihitaji na kugawa, na kama kuna vitu vibovu basi ndio wakati wake wa kuviteketeza.....

Pale ambapo unapopanga mikakati yako ya kimaendeleo, tusisahau na nyumba zetu.....

Jamani nyumba nazo zinahitaji service.....yaweza kua ni ya kila mwaka, ama ya baada ya miaka kadhaaa....ni wewe mwenyewe ndio utaangalia nyumba yako iko katika hali gani.....

Tumekua tukijisahau sana kwa upande wa kufanyia service nyumba zetu.......na mwisho wa siku unakuja kukuta matengenezo yanakua ni gharama zaidi ya matarajio yako..........wakati ungekua unafanya service ungeepuka tatizo hili la gharama mara dufu......