Tuesday, November 19, 2013

FORONYA ZINAPATIKANA HOMEZ DECO........MATERIALS KUTOKA UK NA UTURUKI.....KARIBUNI......


 Size ya foronya hizi ni 45 by 45 na mito pia inapatikana. Mito hubadilisha muonekano wa makochi yako na hupendezesha......
 bei ya kila foronya ni 12, 000.










Monday, November 18, 2013

KAZI YA KUWEKA TILES NYUMBA IKO KIBAHA......

 Homez deco umepata kazi katika nyumba hii iliyoko kibaha ya finnishing ya nyumba nzima mpaka ikamilike.
 Tuliaanza kwa kufanya window shopping na mteja ya tiles katika maduka na tukaipata hii design ambapo wote tulikubaliana tuiweke hii aina ya tiles kwa ushauri wangu.
 Ukiangalia kwa mbali hatujaweka scarting maana tutaweka ya mbao nyunba nzima.

Hebu fikiria nyumba hii ile scarting ya mbao tukiweka nyumba itanogaje.

Nyumba hii imeanza kujengwa tokea mwaka 2012. Na mteja wangu yuko makini kwenye swala la finnishing na tokea kwenye ujenzi kwa ujumla. Na ndivyo inavyotakiwa iwe. La sivyo kwa haraka haraka mnooo. Nyumba huaribika kwa finnishing mbovu. Na sisemi uchelewe sanaaaaa. Ni wewe mwebeyewe na uamuzi wako.


Nashauri utumie wataalamu kwani tutakushuri vizuri kadri tunavyoelekea katika kila stage.

Wakati tunaweka tiles mafundi walikua 7 na niliwagawanyisha kwenye kazi. Na ilibidi walale huko huko site. Ilituchukua siku 5 kumaliza kuweka tiles. Na kuna naeneo machache sana ambapo ni vyooni na jikoni na kumalizia vibaraza kidigo.

Na siku ya leo tuko njiani tunatokea kibaha . Tunakwenda kuangalia tilea za vyooni. Jikoni na mabomba na masink.

Hatua itakayofuata ni kufanya skimming  nyumba nzima ndani na nje na kuweka tiles sehemu zilizobaki.


Nawakatibisha wote kwa mahitaji ya kufanyiwa finnishing na homez deco.

Tutaendelea kuwaonyesha nini kunaendelea...

Saturday, November 16, 2013

SOFA SET INAUZWA...............INA MWEZI MMOJA TUU TOKEA INUNULIWE.....NI MPYA KABISAAAAAAA


 Sofa hii inauzwa kwa bei ya 2,900,000/-    ilinunuliwa Orca Deco, sasa anaeuza kwa bahati nzuri anahamishwa kikazi nje ya nchi........sofa iko katika hali nzuri kama inavyoonekana...na tokea ainunue amekaa nayo mwezi mmoja tuuuu.Color ni Dark brown, purple na cream....


Ni sofa ya watu 3,2,1......
Kwa mahitaji ya sofa hiiii wasiliana nasi kwa namba 0713 - 920565.......bei ni hiyoooooooo..........tayari imeshashushwa.....



Kwa mahitaji yako ya kuuza vitu vya majumbani ambavyo viko katika hali nzuri wasiliananasi....Homez Deco.....0713-920565 ama email: sylvianamoyo@yahoo.com

Wednesday, November 13, 2013

FINNISHING YA NYUMBA ZETU........



Wengi wetu tumekua tukidhani kua kazi nzito ni ujenzi wa nyumba na sio finnishing,,,,naomba kuwaeleza leo kua sio kweli kwa asilimia flani........

Jamani finnishing ya nyumba ni gharama kuliko ujenzi....tutambue hilo, na utakuta wengine mpaka miaka kadhaa hawajamaliza, kwa kua wanajua nini wanafanya ...

Kinachohitajika ni kujipanga, na kutafuta mtaalam aweze kukusaidia katika hili....unaweza kujenga nyumba yako vizuri...lakini ukija kwenye finnishing unaanza kubania hela na kutaka virahisi...yaani jua kua nyumba unaiharibu na hutokua umefanya kazi yoyote ile......nyumba itakua mbaya mbaya na unaweza kujuta.....


Tujitahidi katika hili kua kama najenga nyumba yangu basi ni afadhali nifanye taratibu kwa ufasaha kuliko haaraka haraka na ukaharibu kazi......

Tujitahidi kua wavumilivu katika kumaliza nyumba zetu kuliko haraka haraka, ninasema hivyo kwa kua nakutana na watu kama hawa, na kwa kweli katika kazi yangu sipendi haraka ya kupitiliza kabisaaaaa.......

Kazi ya designing inahitaji muda na nafasi. bila hivyo ni kuharibu kazi.....nami sipendi hilo litokeeee....

Kwa kwetu Tanzania bado tuko nyuma katika hili ingawa tunajikongoja na tutafika kwa kuelimishana na kuelewana...




Sasa hivi vifaa ama vitu vinapanda bei kila kukicha na viko vingi mno ni wewe mwenyewe kuchagua nini unataka na nicha cha wapi kitumike....

Sababu ingine utakuta unamwambia mteja kua hapa panahitajika hiki na hiki, halafu mteja anakua mbishi....oooohhhh hela nyingi mara sababu hiiiikatoa....sasa jamani unavyokataaa fundi afanyaje? na nyumba ikiharibika utamlalamikia fundi sio......unasahau kua ulikua mbishi.......

Mara nyingi mafundi wazoefu wanajua kipi kizuri na kipi kibaya, yaani kama wewe ulivyo kazini unajua kipi kizuri na kipi kibaya. Sasa usiposikiliza ushauri na kutaka ufanyavyo kazi ikiharibika usilalamike.....

Napenda kutumia msemo huu: RAHISI GHARAMA......

Asilimia kubwa kati yetu hua tunapenda vitu vingi rahisi kuliko vitu vichache vinavyodumu na vizuri.....(ntakuja kuliongelea siku ingine)

Homez Deco kwa kweli hatufanyi kazi ili mradi kazi iishe tuchukue hela........tunatoa ushauri kwa mteja.kwanza  na kama   anataka ilimradi iishe basi hua kazi hatufanyi, maana mwisho wa siku ni kuharibu jina letu, na muda wetu.....

Inafika mahali tuambizane ukweli sasa.....

Kitu kingine nilitaka kusahau, jamani baadhi yetu tumekua tukiwabana sana mafundi katika malipo, kitu ambacho si haki hata kidogo, na ndio maana utakuta mafundi wengine wanakuachia kazi, ama wanafanya vibaya kuharibu....etc.   Nashauri tuelewane na mafundi kwa kazi utakayompa na mkubaliane.. na akimaliza kazi yake basi mmalizie hela yake....wateja wengine hata kumalizia hela ya fundi inakua tabu na kazi keshafanya......(ni malalamiko ya mafundi baadhi nilioongea nao)


Naomba tubadilike na tutengeneze nyumba zetu vizuri na ziwe zinavutia na kutazamika na utakaa kwa amani, hutokua na kurudia rudia mara kwa mara.....ni kupoteza hela ambapo ungeitumia kwa vitu vingine.


Tuesday, November 12, 2013

GRILLS DESIGN......

 Tunayo furaha kuwatangazia kua tumeanza kutengeneza grills za madirisha na milango.  Hizi ni baadhi ya designs tulizonazo, na tutaendelea kuwaletea designs nyingi kadri tuwezavyo......

Karibuni wote.........

TUNAOMBA JIBU LA SWALI LAKE KWA MDAU MWENZETU........

Naomba mnisaidie jinsi ya kuosha madumu( vyombo) vya kuhifazia maji, nimetumia njia mbali mbali but naona bado ile rangi ya kijani imekataa kutoka, yanaoneka machafu kweli coz ni meupe na mkono haupenyi ndani..
thanx, mdau wa Arusha.



Monday, November 11, 2013

KWA WALE WOTE WENYE WATOTO WATUNDU WANAOCHORA MAKOCHI........RANGI ZINAZOFAA ZA MAKOCHI.....

 Habari za muda kidogo wadau wangu, nilikua kimya kutokana na majukumu ya kifamilia kidogo, na sasa tuko sawa.

Sawa, sasa kuna tatizo kidogo, kwenye uchaguzi wa makochi ya kwenye nyumba zetu, kwa wenye familia ya watoto wadogo, kwanza kabisa ninachoweza kusema ni kua mtoto ukimfundisha anaelewa, na ukimdekeza atakupa hasara..........sasa ni wewe tuu uamuzi wako.......

Nimekutana na tatizo hili la makochi kuchorwa chorwa na watoto wetu, na jamani bei za makochi tunazijua zilivyo gharama........na pia kwa kua tuna watoto basi hatuna budi kununua makochi ambayo rangi zake ni dark na sio light.......kupunguza tatizo la watoto wetu kuchora kwenye makochi yetu.....

Hebu fikiria umenunua kochi lako kama ndio off white ama cream then likachorwa chorwa na mtoto, kama ni cartoons ama ndio anajifunzia homework etc......


 Nimejaribu kuleta baadhi ya rangi hapa ambazo hazitaonyesha uchafu wa kuchora wa watoto wetu.......
na kwenye accessories ndio unaweza kuweka rangi ambazo ziko light maana itakua rahisi kuzi maintane na kusafisha ama kufua......

 Ninaomba kuwasisitiza wadau kuwafundisha watoto wetu kua hawatakiwi kuchora kwenye makochi, ama ukutani.......na hili linawezekana kabisa...watoto wanaelewa ukiwafundisha.......(mbona shuleni wanaelewa na wanafaulu....sasa itakua nyumbani kuwaelekeza kua wasichore makochi na ukuta etc)

JIBU KWA MDAU







Naomba kumjibu mdau wangu aliyekua ananiuliza kua hii meza ipo.na jibu ni kua meza ipo, na imebaki moja tuuu.....bei ni 1,250,000/=

Karibu tuwasiliane, na samahani kwa kuchelewa kukujibu kutokana na sababu zilizo nje ya uwezo wangu.





Monday, November 4, 2013

TOILET PAPER HOLDER & 2 IN 1 HOLDER

 2 in 1 holder 65,000/-


2 in 1 holder 85,000/-

Toilet paper holder 20,000/-

NB:

All racks without magazines, and toilet paper.