Tuesday, September 24, 2013

MALI MPYA ..........ZINAPATIKANA HAPA HOMEZ DECO.......WASILIANA NASI KWA MANUNUZI - 0713 - 920565

Tunapenda kuwaarifu wadau wetu, wateja wetu na wote kua sasa Homez Deco tuna mali mpya ya sofas na meza za Tv za kisasa........

 Sofas zote bei ni 3,400,000/-  ( bila kusahau discount ipo....)
 Hizi ni sofas zote tulizo nazo.......kulingana na mahitaji yako na space uliyonayo........



 Hizi ndio meza za tv tulizo nazo.......bei ya kila moja ni 1,250,000/-




Tunapenda kuwakaribisha wote.........

NB:
Kutokana na ofisi yetu kua ni ndogo, fanicha zote hizi ziko godown, ambapo utakapokuja ofisini kwetu, utapelekwa kuziona, na vitu vyote hivi ni ready made.



Thursday, September 19, 2013

PROJECT IFUATAYO............




HALIMA KIGUA SIKU YA KITCHEN PARTY YAKE.......

 Hii ilikua ni siku ya Halima Kigua.....kitchen party yake........hapa akiwa na baadhi ya marafiki.....kulia ni Jennifer na kushoto ni Faith......akiwa anaingia ukumbini....


 Halima akiingia ukumbini na somo yake.......
 You are so beautifull my best friend....Halima.....ulipendeza mnoooo....


 Kwa kweli ilikua ni siku ya furaha kwetu sote....tena ukizingatia tulisoma makongo high school, basi tulijumuika na kusherehekea siku ya mwezetu.........


Hongera sana Halima.......



Siku ya kibao kata.....
 Halima akiwa na baadhi ya marafiki zake.....

 Mimi na Halima....(best friends)
 Halima


 Halima akiwa na Faith......
 Marafiki wote tulikuwapo kusherehekea siku ya Halima Kigua.........


NB:

Jamani kwa mimi maana ya rafiki hua ninaitafakari kua, ni mtu ambae mtakua nae kwenye shida na raha.....siku zote maishani mwenu......na haijalishi kama mmejuana ukubwani ama utotoni......mnashirikiana katika mambo mengi pia.....kuambiana ukweli, kuto kusimangana, kusemana......etc........

Mtu unakua na matatizo then marafiki wanakukimbia......jamani huo sio urafiki hata kidogo......


Marafiki wa kweli wapo. ingawa ni wachache mnoooo kadri siku zinavyozidi kusonga mbele.......wanazidi kupungua......



 Halima, nimesoma nae shule ya makongo....tulivyomaliza tukapotezana......na tukaja kukutana huku mtaani......kusema ukweli tulivyokua shule hatukua marafiki hivyo ila ni kusalimiana, story kiasi etc,,,,,

Tukaja kua marafiki ukubwani......kwa kweli.....tumekua marafiki wa kweli, na tunapendana....

SHE IS MY BEST FRIEND EVER...........

Nakutakia maisha mema katika ndoa yako......na hakuna binadamu atakayeweza kuivunja bali ni Mungu pekee aliye juu yetu......muamini Mungu katika kila jambo na utaona baraka zake......

Love u.........

RANGI ZA DULUX (10 YEARS GUARANTEE)...........ZIKISUBIRIWA KUPELEKWA KWA MTEJA.......

 Huu ndio muonekano mpya wa rangi za Dulux.....za ndani naza nje.....nikiwa na maana ya wash 'n' ware ama silk na weather guard.

 Rangi hizi hupatikana kwa AUTHORIZED DEALERS ONLY... na hii inaonyesha ni jinsi ambavyo zina ubora na kiwango cha hali ya juu na hakuna mtu ataweza ku cheza nazo..........
Homez Deco tutawaletea picha ya nyumba ambayo imepakwa rangi hizi.......


NB:
Napenda kuwashauri kua rangi zetu ni nzuri na hudumu kwa miaka 10 tangu umepaka katika nyumba yako ama ofisi yako etc.....inahimili hali ya hewa yoyote ile.....ikipakwa kwa utaalam na kufuata maelezo.

Karibuni sana Homez Deco katika manunuzi ya rangi....na tutakushauri bure......rangi ipi itumike wapi na itaendana na rangi ipi........

Monday, September 16, 2013

MILANGO NA FREMS ZAKE......

Katika nyumba zetu wakati tunajenga, hua tunafanya maandalizi ya milango na frem.....na katika hili inategemea na wewe mwenyewe unahitaji milango ya ina gani? kama ni mbao, alluminium, ama imported etc.......

Nimeona tuongelee kwenye milango na frems zake......zamani tulikua hatujali sana katika finnishing za nyumba zetu, ila sasa mambo yameendelea na technology pia inazidi kusonga mbele. karibia kwenye kila kitu.

Fashion pia haiko nyuma katika finnishing ya nyumba yako, na kila kitu kinakwenda na mpangilio na aina yake na kwa urembo wake......sasa tusidharau milango. kuanzia wa mbele ya nyumba mpaka mlango wa nyuma ya nyumba.....


Tanzania tumejaaliwa kua na misitu, na mbao za kutosha.......na tunao mafundi wazuri pia, na mafundi hawa hupatikana ukituliza akili, na kuvuta subira, ama tunapokwenda kwenye nyumba za wenzetu na kukuta kitu kizuri, usione aibu ama kuogopa kuuliza kwamba kafinyiwa kazi na nani...ili nawe uweze kumtumia na akakutengenezea kitu kizuri.......
Nime weka picha tofauti za frems za milango ambazo tunazo majumbani mwetu......miti hii hii tunayotengenezea, mkongo, mninga etc........yaweza kutokea vizuri ama kutokea vibaya kwa uzembe tuu wa fundi........ama kwa tajiri mwenyewe kutaka kumbana fundi katika kulipia gharama, lakini anataka kitu kizuri.......
Na katika hii hii milango yetu, jamani tujitahidi mafundi wasichafue frems za milango, kwa kua kazi ya milango ni ya fundi wa rangi, basi fundi mason (fundi tope) anaichafua chafua kwa haraka zake, za kutaka kumaliza kazi mapema........ilimradi tuu... ama ana kazi nyingine sasa anataka kuziwahi sizimpite........

Huu ni uchafu wa hali ya juu, na inakuingiza wewe mwenye nyumba gharama ya kulipia kuzisafisha, maana hizi frems, zinarukia cement, etc........

Ukiangalia nyumba hizi zote hazijapigwa rangi, lakini, uchafu unatofautiana baina ya frems na frems.

Ndugu mdau nakuachia wewe ujionee na uangalie ni frems zina gani ambazo zinapendezesha nyumba ama zitapendezesha nyumba yako na kuonekana kisasa zaidi.............

HARRY & HARRIET'S WEDDING.....


Ilikua ni siku ya furaha kwa Mr & Mrs Harry....katika sherehe yao ya harusi..iliyofanyika Hellenic Hall

 ....na hapa ni maids wakiingia ukumbini kwa style...na wakicheza

 Maids wakiingia ukumbini.....
 Bibi harusi akiwa nje ya ukumbi kabla ya kuingia.....
 Maids wakimsubiria  maharusi.....
 walianza kuingia watoto.......kwa mbalii Jossayanne.....akiwasaidia watoto
 Bibi harusi akiingia ukumbini na baba yake mzazi. na alimkabidhi kwa bwana harusi....Mumewe....
 Mr. & Mrs Harry...
 Wageni waalikwa
 Mama wa bibi harusi
 Maids.....kwa nyuma ni Jossyanne
 Kwenye stage, maharusi

 Ulifika muda wa kukata cake......
 Maharusi wakilishana cake

 The kiss after the cake....
 maharusi waliwalisha matron na patron........
 Wazazi wa bwana harusi wakipewa cake....
 Wazazi wa bibi harusi wakipewa cake




 Ulifika muda wa music........

 Nadhani mtakua mnajua wanacheza wimbo gani wa steps....maana hua hauwezi kukosa harusini........


 Maharusi walibadilisha nguo......


 Na hapa ni kipindi cha zawadi......


 Mheshimiwa Rugimbana, alikuwepo na familia yake.....

Na mwisho ni picha ya pamoja na wazazi wa pande zote mbili...........