



Picha za ukutani ziko za aina nyingi sana, na wengi wetu tunapenda sana picha mie mmoja wapo. ila wengi wetu hatujui jinsi ya kuzi ning'iniza picha hizo kwani utakuta ukuta una matundu matundu ya misumari ndio ujue hapo kazi ya picha ilikuwako.
Kuna step 4 za kufuatwa kabla ya kuning'iniza hizo picha na haijalishi ni picha gani wadau wangu. Vitu vinavyohitajika ni:
Steps:
Jamani wengi hatujui maana ya ukipewa ua moja lamaanisha nini! Tumekuwa tukijua baadhi tuuu.
Sasa leo nimeonelea nitoe mada kidogo ya hizo maana.
Ua moja jekundu - nakupenda
Ua jeupe - hisia zangu za dhahiri
Ua la njano - unaleta furaha kwenye maisha yangu naomba tuwe marafiki
Ua la pinki - nimevutiwa na wewe
Ua la rangi ya chungwa - najisifu kuwa na wewe
Ua la peach - asante, ninaomboleza na wewe
Ua la lavender - nimekuhusudu
Ua la bluu - kukipata ni kama ndoto
Kijani: Kutengwa, kukua, hela, mafanikio, utajiri, uponyaji wa mwili, ndoa, uzazi, kazi, balansi, kichochezi cha ukuaji, mafanikio ya kifedha, kutakiana kheri, kazi mpya, mavuno mazuri, love etc.
Njano: Busara na heshima, vitendo, kuvutiwa na ubunifu, kusoma, uwezo wa akili, umakinifu, kumbukumbu, mvuto, kujiamini, furaha, mabadiliko, usalama ect.
Nyekundu: Nguvu, mapenzi, ulinzi, upendo, moto, uzazi, upendo wa mwili na matamanio, kujipa moyo, mvuto, uhitaji, etc.
Nyeupe: Ulinganifu wa rangi zote, mwangaza wa kiroho, usafi, uponyaji, utafutaji wa ukweli, kutokuwa na hatia, umoja, amani, ukweli, ulinzi, uponyaji wa hisia, huondoa mtazamo hasi etc.
Pinki: Upendo, urafiki, mapenzi, heshima, ukaribu, kukaribisha ushirikiano, upendo usiokuwa na kikomo, umakinifu, rangi ya kike etc.
Dhahabu: Mwangaza, ulinzi, mafanikio, utajiri, hela, uanaume, mgawanyo, ushindi, bahati etc.
Lavender: Hali ya kiroho, uchangamfu, kuvutia usaidizi wa kiroho, uwelewa, usaidizi, udhihirisho na kutokuwa na ubinafsi etc.
Bluu: Mawasiliano, ukweli, amani,utulivu, uelewa, busara, ulinzi, uvumilivu, furaha, afya, utiifu etc
Rangi ya Chungwa: Mafanikio, malengo, mvuto wa vitu vizuri, husafisha mtazamo hasi, tukio na mahali, makubaliano ya kibiashara, mabadiliko ya ghafla, nguvu, kuvuta mafanikio, inavuta marafiki, inatia moyo etc.
Brauni: Kukuza mafanikio ya kifedha, ulinganifu wa rangi, inasaidia kutafuta vilivyopotea, nyumba, maajabu ya wanyama, urafiki, maajabu ya dunia, etc.
Papo: Inatumika na rangi nyeupe kupunguza ung'aavu, meditation, kujiamini, maarifa yaliyofichika, ukuzaji wa ulichonacho, kutambulika kazini etc.
Waridi: Kuona huruma kwa mwenyewe na wenzako, nguvu, moyo mkunjufu, msamaha, ubunifu, uvumilivu, mapenzi, uponyaji, etc.
Peach: urejeshwaji etc.
Violet: Nguvu, mafanikio, ubunifu, uhuru na mafanikio ya kifedha na uanzishwaji wa mahusiano mapya na wengine,
Ivory: Ulinganifu, usiokuwa na madhara, kawaida etc.
Nyeusi: Ulinzi, kuharibu uovu, etc.
Silva: Uondoaji wa nguvu hasi, ushindi, uthabiti, kuondoa, etc.
Wote tunaijua mishumaa, iko ya aina tofauti tofauti inayotoa marashi na ambayo haitoi. Na kuna inayodondosha maji na isiyodondosha maji.
Mishumaa hutumika kama mapambo majumbani, hutumika pia gizani, sherehe mbalimbali na nyumba za ibada etc.
Kuna rangi mbali mbali za mishumaa, leo nimeona nielezee baadhi ya rangi hizo na maana zake.
Mishumaa hii ikitumiwa bila uangalifu hatari, yaweza kuwa chanzo cha moto.
ONYO: USIACHE MSHUMAA UNAWAKA BILA UANGALIZI, USIACHE MSHUMAA KARIBU NA WATOTO NA WANYAMA KAMA PAKA, MBWA etc. USIWASHE MSHUMAA KARIBU NA KITU KINACHOWEZA KUSHIKA MOTO KWA URAHISI. HAKIKISHA UNAWASHA MSHUMAA MAHALA AMBAPO HAPAWEZI KUSHIKA MOTO HARAKA HATA KAMA UKIISHA.
Leo nimependelea tuongelee kuhusu mapazia. Kwenye sekta hii kidogo kuna ka ugumu kwani watu wengi huwa wanadhani ilimradi pazia tuuu. Mapazia yalianza kutumika tokea karne ya kumi na tisa. Nia ya mapazia kwanza ni kuzuia mwanga wa jua kuingia ndani, vumbi, na kuzuia watu wa nje wasione ndani wakati wa usiku na kupendezesha nyumba etc.
Mapazia yanaweza kupendezesha nyumba ama yanaweza kuharibu muonekano wa nyumba. Naomba kuwakumbusha kuwa kuna mapazia ya aina 2. Mepesi na Mazito. Muangalie na Texture ya mapazia.
Mapazia yako yaliyotengenezwa kabisa na kuna ya kuchagua kitambaa kikashonwa.
Sehemu za baridi ni vizuri kuweka mapazia mazito na za joto weka mepesi. Nikisema mepesi sio yale ya kuanganza ndani bali vitambaa vyake vinakuwa sio vizito sana.
Kwenye dirisha kunatakiwa kuwe na mapazia mawili, jepesi linalosaidia kuzuia vumbi ndani, na la kawaida liwe zito zito kiasi kama ni kwenye joto na baridi liwe zito.
Kwa upande wa rangi ya mapazia jitahidi rangi ziwe zinashabihiana, kuna yaliyo na marembo na mengine hayana urembo wowote.
Sasa kuna dizaini nyingi sana za mapazia, yaweza kutumia katein boxi, vimbao vidogovidogo vya curtain poles nisaidieni kiswahili, kuna ya mbao zinazofunguka, aluminium etc.
Tengeneza mapazia kutokana na dirisha lako lilivyo. Madirisha ya jikoni, stoo, ofisini na chooni ni vizuri ukaweka mapazia mafupi. Kuliko baki weka mapazia marefu na weka kambaa mahususi kwa kufungia pazia au vichuma vinavyogongewa ukutani vya kufungia wakati wa mchana.
Vipimo pia jamani vinamata hapa usiweke pazia mpaka likaburuza chini.
Kuna dizaini za mapazia ya nyumba kubwa na nyumba ndogo, msichanganye hapo maana nyumba itaonekana kituko.
Napenda kuchukua fursa hiii kuwashukuru wote. Nimekuwa nikizisoma comments zenu na nimefurahi sanaaa.
Ninachoweza kusema ni kwamba kwenye hii blog msisite kukosoa pale ambapo mnaona panahitaji marekebisho kwani mimi ni mdogo wenu,dada yenu etc, nina mapungufu pia na kwa kufanya hivyo tutasaidiana kwa kuelimishina. Hii ni blog ya kuelimishana.
Kuna mdau mmoja anasema kuwa niwe naweka vitu vya bongo zaidi, kwa hapa naomba nimwambie kuwa, blog hiii haiko kwa vitu vya kibongo tuuu bali ni vya dunia nzima, mtakubaliana na mimi kuwa tunahitaji watu tubadilike na twende na wakati.
Na niko mbioni pia kuna ka program kanakuja kwa atakeyekuwa tayari anaweza kunipigia simu na nikaja nyumbani kwake nikapiga picha na kuziweka kwenye blog bila malipo na ni kwa Dar tuuu. (KWA ATAKAYE KUWA TAYARI).