Sunday, December 20, 2009

upangaji wa bafuni, au maliwatoni

Jamani sio kila kitu kinakaa kwenye dressing table, mimi sina mengi ya kusema, Mrs. Jossanne ameshaongelea, na umejionea ukihifadhi vitu kwa usafi na mpangilio basi na nyumba,ofisi etc. kutakuwa kusafi. Tueite Kreative Homez (Homez deco) na tutakusaidia. (Sylvia - Homez deco) She is Cute is she?


Wakina mama, wakina dada, wakina baba usafi ni kitu cha muhimu sana, especially linapokuja
la bafuni na kwenye vyoo tunavyovitumai viwe vya kukaa, au kuchuchumaa, lazima usafi upewe kipaumbele iwe nyumbani, ofisini, kiwandani hospitalini, mashuleni, madukani, usafi usafi ni jambo ambalo baadhi ya watu hawajali vyoo kuwa visafi au bafu.

Ikumbukwe kwamba magonjwa ya maambukizi, magonjwa ya zinaa yanaanzia huku, Nijukumu la kila mmoja make sure sehemu unayojisitiri ni safi, maji unayotumia makopo munayotumia vyooni, yawe masafi siku zote kuna vijidudu ambavyo havionekani kwa macho ni hatari sana,
hasa kwa sisi wakina mama, wakina dada lazima tuwafundishwe, watoto, kunawa mikono, kila mara, una toilet ya kawaida iwe safi, weka dettol kwenye maji kill bacterias.

Wakina mama, wakina dada ni reseach nyingi sana zimefanyika kuhusu kansa ya mlango wa kizazi mara nyingi ni uchafu, hata ktk nchi zilizoendelea, kwa suala la usafi ni la kwetu wote si la DC, AU RC SERIKALI ZA MITAA, UNA JIRANI MCHAFU MWAMBIE TUACHE KUONEANA AIBU, WENYE NYUMBA AMBAO HAWANA, VYOO VYAO VIMEJAA WARIPOTIWE MARA MOJA, USIPANGE NYUMBA AMBAYO INA MATATIZO YA VYOO, MABAFU, NAWATAKIA X-MASS NJEMA WOTE, mzingatie hayo tutakuwa tukielimisha ktk makala mbalimbali, asanteni.

No comments:

Post a Comment