Thursday, December 3, 2009

Mazungumzo kati yangu na Mrs.Jossyanne George muda mfupi uliopita kupitia kwa email

Sylvia - Homez Deco says:

hi sis,

pole na kazi, sasa nimezitoa kazi zako kwenye blogsite yangu, tuwe tunawasiliana na pia nina idear moja kuwa at least kwa wiki mara moja uwe unanitumia article kuhusu landscaping kwa ajili ya kuelimisha nami nitai publish, kwani huku watanzania wenzio wamekukubali sana.

na pia ninafikiria mwezi wa nne ukija tufanye kama get together na baadhi ya wadau wetu huku uwape somo na wao wakuulize.


au kama una idear ingine nzuri nijulishe itakuwaje.

kazi njema, and please get back to me as soon as possible ili tuwe na muda mrefu wa kutangaza na tupate feedback nzuri.

karibu.

Mrs.Jossyanne George says:

nitajitahidi dear, nikija tukae chini tuelekezane, vizuri, ila asante sana, kwa kuwaelimisha watanzania wenzetu maana, wote hatuwezi kuwa ma engineers, doctors or mis pageants, au madegsners,

inabidi tuangalie na mambo mengine ya kufanya ktk maisha,na kimaendeleo, unajuwa uwa ninajiuliza ili suala la usafi wa mji wa dar ni aibu na si suala la serikali, ni la sisi wote kusadiana, kuanzia kwenye mashuleni, mpaka vyuoni, nikuelimishana,utunzaji wa mazingira yetu kutotupa taka ovyo watu wanatupa machupa ovyo.

mifuko sewerage systems za dar hazina service yoyote, mvua ikinyesha dar foleni masaa 6 hakuna anayeona hii kero, watu wanafungulia vyoo, milipuko ya magonjwa
huu .wote ni uchafu, uchafu, inasikitisha sana,

kila leo watanzani wanasafiri nje ya nchi ina maana ni vipofu, dada tunaweza kuwa na magari ya kifahari, majumba, mazuri, tukavaa nguo za madesgners ila tunaishi ktk mazingira, machafu ya milipuko ya magonjwa

jibu ni kwamba wote sisi ni wachafu, no body care, ni mzee MENGI ndie anaepiga kelele siku zote na baadhi ya viongozi tuone aibu mji wadar ni mchafu ni aibu kwa wakazi wa dar, wote,

tunaweza kuchangia maharusi, clubs, za michezo kwanini tusichangie kusafisha mazingira? kuokota taka tukawa na mpangilio mzuri, asante sana dada mungu akulinde

chaoo!!

Hayo ndio yalikuwa maongezi yetu kupitia email.

Tunakaribisha michango yenu ya mawazo juu ya hili swala la mazingira, JE TUPANGE SIKU TUWEZE KUELIMSHANA JUU YA USAFI WA MAZINGIRA KUANZIA MAJUMBANI MPAKA JIJI LA DAR NA HATIMAE TANZANIA NZIMA? KUMBUKA HUYU NI MTU ALIYE SPECIALIZE KWENYE LANDSCAPING.

No comments:

Post a Comment