Sunday, December 20, 2009

KUHUSU SUALA LA USAFI, WA VYOO, MABAFU NK

Mi binafsi ni mpenzi wa blog hii, inahelimisha sana, nyanja fotauti, mazingira tunayoishi, majumbani kwetu, usafi kwa ujumla,maofisini, sehemu za biashara, madukani, sokoni, Ila watanzania waliowengi swala la usafi, vyooni na bafuni hawalipi umuhimu, hata kidogo, kuna baadhi ya ofisi ukiingia kwenye bathrooms zao, unaweza kupata heart attack, ukalazwa uchafu uchafu.

Kama ulivyotoa kwenye blog hii hivyo vyoo, hizo sehemu zipo na nyingine ni mahotelini, kuanzia reception, vyumbani, unaenda kuonyeshwa rooms unakutana , na panya, mende, vumbi, buibui jamani inakuwaje mnaweza kujenga majengo, au nyumba za wageni ila suala la usafi, hamlipi kipaumbele???

Mara nyingi nimeona, wengi wenye mahoteli, hamtoi ajira kwa watu ambao wamesomea hotel management, mnatoa ajira kwa sababu ni mtoto wa ndugu, jirani, au girlfriend wako acheni hizi tabia zinacost sana, tu.

Pia acheni ubahili wa kugaramikia, vitendaea kazi, kwa wafanyakzi wenu, nunua, vitendea kazi, kama vile gloves,detergents, masks, pia wenye mahotel wengi ni wabahili wakulipa mishahara mizuri , mko radhi muwende kwenye mabar kuosha majina, ila sehemu zenu ni uchafu uchafu uliopitiliza, na kwanini hakuna mabwana afya wa kukagua hizi sehemu mpo mnapokea rushwa, tu hamjali maisha ya watu.

SEHEMU NYINGINE NI MAOFISINI ni aibu bathrooms zinatisha, nobody care kwasababu ofisi, ila nataka kuwaelimisha ndugu zangu wafanyakazi nyinyi ndio kutwa nzima mnashinda hapo mnaenda haja kubwa na ndogo kwa kutumia vyoo hivyo na magonjwa ndio mnavyoyazoa, huku vyooni, lazima hizi sehemu ziwe safi, ni hatari sana kwa afya zenu.

Ninawashauri, wakina mama, wakina dada, wakina baba, sehemu zenu za kazi, ziwekeni safi kuna kila aina detergents zinauzwa kwenye super markets, srubers, blushes, vim, kama kuna mtu anayesafisha hizo sehemu make sure ana vitendea kazi.

Baadhi ya magonjwa yanapatikana, kwenye hizo bathrooms ni U T I, MAGONJWA YA SEHEMU ZA SIRI. hayo makopo munayoweka vyooni yasafishwe, kila mara wekeni dettol kwenye maji maana, kuna vijidudu ambavyo avionekani kwa macho, naweni mikono siku zote, pia kuna wakina dada ,wakina mama, tunaelewa sisi monthly periods, tuelewe na kuzingatia usafi umetumia choo, safisha, usitupe hovyo, pad, tempons, au aina yoyote ya vipande vya nguo choooni ni mwiko unajuwa uko kwenye MP nenda namfuko wako badilisha weka kwenye mfuko tupa kwenye dustibin pia wekeni vikapu vya ktupia uchafu, wekeni mfuko ndani ya kikapu au dustibin umejaa funga tupa sehemu inayotakiwa.

WAKINA BABA nyinyi tatizo lenu, ni kukoja chini hii nitabia mbaya sana, kutupa condoms ndani ya vyoo jamani mnasabisha vyoo kuziba, umepost barua zako makesure zimeenda panapotakiwa, isiwe kero kwa msafishaji mpoo mnaofanya makusudi mazima, mnaeleweka tabia zenu acheni mi kama ninakujua nakuambia ukweli.

Pia wakina kaka , wakina baba, tabia ya kukojoa hovyoo barabarni kwenye vichochoroni, mbele ya wakina mama wakina dada ni tabia mbaya zinatakiwa kutungwa sheria za watu kama hawa, kushikiswa adabu mnashindwa na wanyama hamuoni paka akikojoa hovyo au haja kubwa iweje mnyama awe na akili ya kujihifadhi ???? nyinyi watu wazima, mshindwe? Shame on you

from Mrs. Jossanne Geogre.New York Marekani

No comments:

Post a Comment