Monday, May 27, 2013
Muendelezo wa matayarisho ya ukuta na kupaka rangi......nyumba ya kinondoni.......
Picha hizo mbili juu nikionesha jinsi gani vumbi linabaki ukutani baada ya kupiga msasa mlaini kuondoa rangi iliyochakaa.....na hapo ni baada ya kulifuta kwa ufagio zile za ndani.....lakini bado vumbi liko......sasa hebu fikiria, na vumbi hili lililobaki halafu unapaka rangi juu yake....hii rangi kamwe haitaweza kukaa kwa muda unaotakikana, maana vumbi ni sumu ya rangi...
Picha hizi mbili za juu ni baada ya kupaka sado binder ni gundi ambayo husaidia vumbi lisikutane na rangi na hufanya rangi kudumu kwa muda mrefu bila madhara ya kubanduka ama kuchakaaa....gundi ziko za aina mbili kuna sado binder ama bonding liquid ambapo zote zinafanya kazi sawa ila hii bonding liquid ina uwez zaidi...sasa ni mfuko wako tuuu.......hapo nikiwa nimeridhika na kazi ya mafundi na ndio nimewaruhusu kupaka hii gundi tayari sasa kwa kupaka rangi.....ya dulux katika sehemu zilizokusudiwa.....
hii ndio gundi sado binder ambapo matumizi yake ni kua kama utatumia lita nne itabidi uongeze maji ya lita nne na kama ni ndoo moja basi ongeza maji ndoo moja.....ndio uweze kupaka ukutani...ila kwa bonding liquid haihitaji kuchanganywa na kitu chochote kile ni moja kwa moja unapaka ukutani........
nikiwa natafakari jambo hapa......hhahaah, hahhaha........wakati mafundi wakiendelea na kazi ya kupaka rangi.....rangi hizi hazina harufu.......
fundi akipaka rangi kuta....na tulipaka sitting room, corridor na dinning......tunapaka kwa awamu......
Rangi za dulux ni zinapakwa koti mbili tuuu. na inafunga kabisa ukutani......nyumba hii ilikua na skarting ya dark brown.....na tulivyopaka rangi zetu iliziba kabisa....yaani hata huoni kama kuna rangi ya brown ilikuwepo.........Unaona jinsi ukuta unavyovutia........
najua mtakua mnajiuliza ninafanya nini ama ninapima nini.........Katika interior design......fanicha zinaingia kwa vipimo.....wengu wetu hua hatujui hilo....na ndio maana utakuta mtu nyumba ni ndogo, lakini kajaza makochi, tv ni over size. dinning table etc.......sasa kwa mteja wangu huyu yeye alikua anatoa fanicha zote alizokua nazo na anataka mpya...na anafanya kwa awamu......na amekubali nimshauri katika ununuzi wa fanicha.......
Hapa nikipima meza yake ya kulia chakula.....meza hii ni yawatu sita.....ina upana wa futi 3.5 na urefu wa futi 7. Wakati dinning ina urefu wa futi 9.5 na upana wa 9 na robo.
Sasa tatizo linakuja kua hakuna nafasi ya kutosha hapa...na urefu wa meza unakaribiana na urefu wa hiyo dinning yenyewe........inakua haileti picha nzuri......Nilicho mshauri ni kua aweke meza ya watu 4.....na pia ukiangalia kwa pembeni hapo dinning kuna samaki wa kufugwa....sasa space inazidi kua ndogo......mteja wangu amekubali ushauri wangu.....na meza ya hao samaki itabadilishwa na kuwekwa ingine nzuri.......
Tutaendelea kesho katika hatua ya mwisho wa nyumba hiiiiii.......................................
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment