Thursday, May 2, 2013
Matumizi ya Gypsum powder kwenye ukuta wa nyumba zetu ama ofisi zetu.....
Nadhani wengi wetu tunaifahamu gypsum powder. Leo nimeonelea kuiongelea kutokana na kwamba hua inatumika vibaya, mahala pasipohitajika kutumika......Katika pita pita yangu kwenye nyumba, wakati nafanya kazi, kupima mapazia, kutoa ushauri etc.......nyumba .nyingi mafundi wanatumia gypsum powder katika kuandaa ukuta kwa matayarisho ya kupaka rangi......
Jamani hili ni kosa kubwa mno.....na wengi wetu tunatumia mpaka kwenye ukuta wa nje ambapo huko sasa ndio hakufai kabisaaaa, maana haihimili hali ya hewa......na matokeo yake nikua rangi inabanduka, ama kuweka cracks kua huu unga unaachiana na ukuta.......Nimejaribu kufanya research ya kwanini watu wanatumia huu unga wa gypsum ukutani......kutoka kwa mafundi wenyewe, na wateja......na jibu nililolipata ni kwamba.....wengi wanakimbia gharama za kununua products sahihi za ukutani, wengine hawajui...etc.....Yaani bora asiyefahamu.....lakini huyu anaekimbia gharama...ndio siwaelewagi kabisaaa....maana kama unaweza kujenga nyumba mpaka ikasimama nani nyumba nzuri....iwe ndogo ama kubwa zote ni nyumba.....kwanini unaharibu upande wa finnishing.... kwa kutaka kuepuka gharama?....yaani ni bora ujenge kwa awamu kuliko kufanya upesi na kuharibu.....jamani hiyo nyumba si ni yako unataka kuhamia? ama hataka kama unataka kupangisha? Kwanini usiitengeneze vizuri......Naomba tubadilike katika hili...na utaona nyumba yako ukipaka rangi inakaa muda mrefu na kudumu.......
Sasa basi ningependa kuchukua fursa hii kusema kua huu unga wa gypsum ni mahususi kwa ajili ya cyling board aina ya gypsum....ambapo ndio mahala sahihi unga huu unatakiwa kutumika.
Somo hili litaendelea.............
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment