Neno la kwanza tukienda kwenye makabati yetu kuchukua nguo ya kuvaa utasikia sioni nguo, ama sina nguo wakati kabati limejaa nguo. Na hii ni kutokana na mpangilio mbaya wa nguo, na ndio maana tumekuwa tukirudia rudia nguo mara kwa mara kwa kujua ama bila kujua. Na wanaoongoza kwa nguo nyingi duniani ni wanawake. Utakuta mtu ana nguo nyingi na anazo zivaa ni chache, na hii hutokana na kwamba hana mpangilio mzuri wa nguo zake. Hakikisha kwamba kabla hujaanza kupanga chagua nguo usizozivaa zitowe, na uzigawe kwani itakusaidia kupata nafasi na kujua ukienda kufanya shopping ununue zipi. Ziko stepu kama nne ama tano ya kupanga nguo.
- Panga nguo kwa misimu kwa wale walio sehemu za baridi
- Panga nguo kwa types za nguo, kama unaona kupanga kwa misimu kwako haiwezekani, basi kuna njia hii ya pili, nikizungumzia types ni kama, mashati, tishet, sketi, suruali etc. kwa njia hii itakusaidia kujua ni nguo za aina gani unazo, na pia itakusaidia kuchagua nguo kwa urahisi, na kujua idadi.
- Panga nguo kwa rangi, hii itakusaidia pia kuchagua nguo zinazoendana kwa urahisi, mfano kama una tisheti ya pink na umeitoa sehemu uliyopanga tisheti peke yake kwa rangi, utaenda ulipopanga sketi, na itakuwa ni rahisi kujua ni rangi gani uchague inayoendana na tisheti ile.
- Kupanga nguo zilizokunjwa, sasa kuna kupanga kwa aina mbili kama kabatini basi panga pia kwa rangi na kwa kuzilaza kama tulivyozoea, ila kama ni kwenye droo basi panga kwa rangi pia ila kwa kuzisimamisha kama ilavyoonekana hapa.
No comments:
Post a Comment