Thursday, September 10, 2009

Jinsi ya kupanga chumba cha mtu mmoja

Nimeombwa kuonyesha vyumba vya bachelor vinakuaje. Sio kwamba nilisahau ila nilikuwa nalifanyia kazi ili niwaletee mambo mazuri.

Vyumba hivi mara nyingi vinakuwa ni vya wastani, hivyo vinatakiwa viwe visafi muda wote kwani hapo ndio chumbani,sebuleni,dinning etc. Hutakiwi kujaza vitu vingi chumbani.

Kwanza: angalia ukubwa wa chumba chako.

Pili: rangi utakayopaka hakikisha itafanya chumba kiwe kikubwa, rangi hizo ni, rangi zilizo bright hufanya chumba kiwe kubwa na zilozo poa zinafanya chumba kiwe kidogo(angalia chart niliyoelezea rangi hapo chini).

Tatu: angalia unahitaji ceiling board(gypsum au ya kawaida) na sakafu ya aina gani, kama ni tiles, ama utaweka carpet, ama cement etc

Nne: angalia wingi wa fanicha zako, hapa sasa ndio huwa panachanganya wengi. Vitu muhimu kwa mwenye chumba kimoja ni: kitanda, kabati la nguo, tv na radio, fridge, shoe rack, jiko, kochi dogo hata la mtu 1 na kameza ama stool inategemea na ukubwa wa chumba. Angalia kama vyote vyaweza kuingia, ila kama haviingii basi, punguza vitu kwa kutumia njia ya 2 in 1. Hii ni, mfano kabati la nguo unganisha na shoe rack, meza ya tv tafuta inayoweza kuhifadhi vyombo, radio na tv yenyewe, kitanda sio lazima kiwe kikubwa. Hapa utakuwa umepata nafasi pia hata ya kupita.

Mwisho: Remba chumba chako kwa picha za ukutani chache hata moja ikiwezekana na saa ya ukutani. 

Siri ya kuwa na chumba kisafi wakati wooote ni: acha kuweka vitu chini ya uvungu, na kila unapoamka tandika kitanda kabla ya kwenda kuoga. Jamani hivi unajua ukiacha nyumba chafu, ukirudi ndio unachoka zaidi? nyumbani kwako ndio sehemu ya kupumzika na kutafakari kuwa kesho inakuwaje etc.

Tumekuwa na ile tabia ya kuwa hatuzipendi nyumba zetu kisa ni ya kupanga. Ukiangalia anayeishi ni wewe na sio mwenye nyumba sasa hata ukipata nyumba yako si itakuwa chafu maana ushazoe kuishi pa chafu? Hii tabia tuiache weka mazingira yako safi.

No comments:

Post a Comment