Nimeombwa kuelezea garden na mmoja wa mdau mwenzetu, wengi tunapenda sanaaa garden zetu, ila kuanza na mahali gani iwe ndio inakuwa ni matatizo. Garden inahitaji uangalizi wa karibu sanaaa na usiwe bahili wa hela, na cha kuangalia baada ya kuamua kuanzisha garden ni:
- Kwanza ujue udongo wako ni wa aina gani
- Kuna maji ya kutosha
- Eneo lako lina ukubwa kiasi gani
- Hali ya hewa pia e.g. joto ama baridi
- Kuna miti mikubwa
- Nyumba yako iko eneo gani kwa jinsi ulivyoijenga (pembeni, katikati, nyumba, ama mbele ndani ya fensi)
Sasa ukisha gundua hili, itakusaidia kujua upande maua aina gani, mpangilio gani na style ipi.
Mahitaji ya kuanzisha garden ni:
- Jembe
- Beleshi
- Wheel baro
- Reki
- Mbolea
- Kamba
- Mkasi
- Gloves
- Overroll
- Buti za plastic
- Udongo (huu udongo hununuliwa una rangi kama nyekundu hivi ama mweusi mweusi) kwa ajili ya kuchanganyia wakati ukiandaa maua kwa ajili ya kupanda)
- Maji
- Maua
- Madawa ya kuua wadudu
Maua yako ya aina nyingi sanaaaa. Kwa hiyo kua mwangalifu sanaaa wakati wa kununua maua kwa ajili ya kupanda kwenye garden yako chagua maua yanayolingana na hali ya hewa uliyopo. kama vile joto, baridi etc.
Maua ya kwenye vyungu, pia udongo, uwe umechangwanywa vizuri na mbolea, ua lilingane na chungu sio chungu kidogo ua kubwa, na yasikae sana juani, tafuta sehemu yenye jua la wastani, na kama unayaingiza ndani basi kila baada ya siku nne mpaka tano litoe nje lipate mwanga, bila kufanya hivyo litakufa.
Maua yote haya yanahitaji kupapaliliwa. Na hakikisha maua yamwagiliwa kwa siku mara mbili. Maua ya liyopandwa kwenye vyungu yamwagiliwe maji kidogo, ukiweka mengi yataoza.
No comments:
Post a Comment