Friday, October 5, 2012
Usafi wa weekend hii...... Kabati lako la vyombo
Leo nimeona tuzungumze kwenye upande wa kabati la vyombo, liwe liko jikoni, ama dinning......yote hayo ni makabati yanayohifadhi vyombo...
Kumekua na tabia kwa wengi wetu... kua tunatenga vyombo vya wageni..... yaani vyombo hivi haviguswi kabisa mpaka aje mgeni...
Tabia hii kwa kweli si nzuri sana, maana hua inafanya hivi vyombo haviguswi, si havitumiki? sasa hata kufutwa vumbi, ama kuoshwa, haviguswi.....
Mtindo huo ni wakizamani, hebu fikiria, umenunua vyombo vyako kwa hela yako mwenyewe, halafu hauvitumii eti mpaka mgeni aje, na akija anatumia yeye mwenyewe.... kweli jamani ni haki hii...
Hii tabia tuiache kama si kupunguza..... kwani husababisha vyombo kua na uvundo, ama kua na harufu za wadudu kama mende, na kuhifadhi mazalia ya wadudu...
Vyombo vyote vitumike kwa utaratibu ulioupanga... na hii itakusaidia kua unajua mitindo ya vyombo vilivyoingia... sio mtu unakaa na fashion ya vyombo vya mwaka 47... mpaka sasa....
Tujirekebishe kwa tabia hii si nzuri kama mnavyofikiria......
nawatakia weekend njema....
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment