Weekend ndio hiyoo tunaianza muda si mrefu, umejipangaje? Kwenda site, shamba, kutembelea ndugu, kupumzika nyumbani, ama kufanya usafi......
Kwa wale watakaokua majumbani, huu ni muda mzuri wa kusafisha na kubadilisha jiko lako kwa siku 1, ni rahisi sana....kumbuka tumekua tukiwaachia wadada wa kazi wafanye kila kitu, weekend hii jitahidi uingie jikoni kwako na msaidiane kufanya huo usafi, na ndio muda wa kujua umebakiwa na glass ngapi, sahani ngapi, vijiko etc..... sio kumgombeza tuu dada mbele za wageni unapomuagiza chombo, then anakuambia kua kimevunjika.......
Hatua ya kwanza, toa vyombo vyote nje, yaani jamani kuna nyumba zingine jamani unaletewa glass inanuka lile vumbi la mende kama vile watu hawaishi kwenye hiyo nyumba lol..... nilishawahi kukutana na hili tatizo siku..... ni aibu.....
Hatua ya pili,
Fanya usafi wa fridge lako, na jiko lako, Futa vumbi kwenye madirisha, toa pazia hilo ufue, makabati yako, na kutoa bui bui ukutani, juu ya dari, makabatini, na kisha fagia na uzoe na kutupa hayo mauchafu, sio ukusanye uweke pembeni, ama hapo mlangoni.
Hatua ya tatu,
Angalia je makabati yako yako salama, hayajachomoka zile handle za milango, bawaba hazijalegea, kama kuna kabati linahitaji huduma ya fundi tafadhali muite na arekebishe, maana huo ndio muda wenyewe, badilisha pia vioovilivyovunjika, kama kunahitaji polish pia mwambie fundi wako apige, akiwahi kupiga asubuhi, mpaka jioni imeshakauka.
Hatua ya nne,
Uwe na sabuni na madawa ya kufanyia usafi, dasta, makosheo etc......
Hatua ya tano,
Anza kufanya usafi wako wa jiko lako, unaanzia juu kuja chini..hakikisha unagusa na kusafisha kila mahali, fridge sogeza, jiko sogeza......fanya usafi wa kila sehemu, usimwage maji chini, maana wengine wanadhani kumwaga maji mengi ndio kufanya usafi, hapana, maana kama una tiles, na maji yako ya sabuni, utapiga mueleka.....Ukuta wako pia ufanyie usafi, kwa kutumia dasta, na usugue taratibu sehemu yenye uchafu, na uwe unazungungusha kama durua wakati wa kusafisha, taratibu, la sivyo utachuna rangi ya ukuta wako.. na makabati usiyamwagie maji, futa na kitambaa chenye maji maji ya dawa ama sabuni kwa mbali.....
Hatua ya sita,
Kausha vizuri, ukuta, makabati yako, ukiridhika, anza usafi kwenye hizo meza ama makabati ya chini,,,, fanya usafi hatua kwa hatua, sio unasafisha kote, halafu unakuja kumalizia, uchafu utaganda kule ulikoanza mwanzo.... maliza usafi wa juu kabisa, halafu uju usafi wa chini, hilo sink lako pia lifanyie usafi wa kina,, kama kuna madasta ya zamani jamani tupa, kosheo la zamani tupa, etc. makabatini,
Hatua ya saba,
Sasa malizia na sakafu yako....na hakikisha hakuna watu wanaopita pita hapo jikoni wakati wewe unafanya usafi........
Hatua ya nane,
Jiko lako si limeng'aa sasa? umeridhika nalo? kama umeridhika nalo, sasa liache lipate hewa...
Hatua ya tisa,
Nenda nje na dada, ama kuna msaidizi mwingine basi mjumuike.....huu ndio muda wa kufanya stock take yako ya vitu vya jikoni, angalia vitu ambavyo huitaji, vilivyovunjika, vilivyochakaa etc, toa weka pembeni, osha vyombo utakavyovihitaji, viache vikauke, kidogo, na ufute na dasta safi, maana hakuna ninachochukia kama unafuta glass then inabaki na nyuzi nyuzi za dasta,, usifute glass ikiwa haijakauka......
Hatua ya kumi na ya mwisho...
Panga vyombo vyako kulingana na rangi, aina ya vyombo, na matumizi ya vyombo.... kwa mtindo huu itakusaidia sana sana kujua vyombo viko wapi ......
Haya umemaliza usafi wako wa jikoni, na furahia jiko lako kua safi, na kujua ya kua nini hauna na unahitaji kununua.
Hauni raha sasa jiko lako kua safi.......na hewa inaingia sasa, na harufu nzuri iliyoko jikoni kwako, na hakuna wadudu hapo?
Nawatakia weekend njema..........
No comments:
Post a Comment