Thursday, August 20, 2009

Vyoo vyetu

Leo nitaingia upande wa choo ndugu zanguni.

Mmh jamani yote tisa kumi ni choo. Hivi mnajua ya kuwa maisha yako utakayoishi duniani, miaka 3 unatumia chooni eitha kwa kuoga etc. (hii imetoka kwa profesa ......... katika utafiti wake)

Choo kina umuhimu wake wajemeni, kina uzuri wake na ubaya wake. Ukikifanyia masihara kinakuletea ugonjwa, ukikijali basi kitakuletea amani nyumbani kwako.

Vyoo viko vya aina nyingi,

  • Vya shimo
  • Vya kukaa etc

Sasa hivi vyote vinahitaji umakini wako, kuanzia rangi, usafi ukarabati etc.  Nimekuwa nikisikia malalaniko sanaaa kwa tunaokaa nyumba za kupanga, utakuta mtu hakikarabati choo mpaka mwenye nyumba, hapa nazungumzia ukarabati mdogo mdogo tuuu jamani msije nitoa macho bure. 

Kuna madawa ya usafi yako madukani kwa usafi wa choo tena yaa aina nyingi na ni ya bei nafuu mpaka ya gharama. Hapa sasa ni wewe tu na mfuko wako, na vitu vitumikavyo chooni lazima visafishwe kila ufanyapo usafi kama ndoo, kopo ect.

Mama yangu alinipa siri ya usafi wa choo, UKIWA NA KINYAA JUA YA KUWA SIKU ZOTE CHOO KITAKUWA KICHAFU NA KUMBUKA NA WEWE PIA HUKITUMIA.

Hakikisha ukimaliza kuoga ama kutumia acha choo kisafi na kikavu masaa yote.

Mataulo pia huhitaji kubadilishwa kwa wale mnaotundika mataulo bafuni na yasilundikane,utakuta mtu kaweka mataulo 4 kwenye henga zile za ukutani za chooni haifai, yatatoa harufu ya uvundo ama vumbi, tenganisha. Kamwe usitundike taulo mbichi ndani kwani litavunda na kuleta harufu mbaya chooni. 

Kumbuka kuweka vitu kama miswaki, dawa zake etc mahala pasafi na salama, inashauriwa tumia mswaki isizidi wiki 3 ubadilishe. Na choo kisafishwe angalau mara 2 kwa siku

Asanteni,

No comments:

Post a Comment