Monday, September 16, 2013

MILANGO NA FREMS ZAKE......

Katika nyumba zetu wakati tunajenga, hua tunafanya maandalizi ya milango na frem.....na katika hili inategemea na wewe mwenyewe unahitaji milango ya ina gani? kama ni mbao, alluminium, ama imported etc.......

Nimeona tuongelee kwenye milango na frems zake......zamani tulikua hatujali sana katika finnishing za nyumba zetu, ila sasa mambo yameendelea na technology pia inazidi kusonga mbele. karibia kwenye kila kitu.

Fashion pia haiko nyuma katika finnishing ya nyumba yako, na kila kitu kinakwenda na mpangilio na aina yake na kwa urembo wake......sasa tusidharau milango. kuanzia wa mbele ya nyumba mpaka mlango wa nyuma ya nyumba.....


Tanzania tumejaaliwa kua na misitu, na mbao za kutosha.......na tunao mafundi wazuri pia, na mafundi hawa hupatikana ukituliza akili, na kuvuta subira, ama tunapokwenda kwenye nyumba za wenzetu na kukuta kitu kizuri, usione aibu ama kuogopa kuuliza kwamba kafinyiwa kazi na nani...ili nawe uweze kumtumia na akakutengenezea kitu kizuri.......
Nime weka picha tofauti za frems za milango ambazo tunazo majumbani mwetu......miti hii hii tunayotengenezea, mkongo, mninga etc........yaweza kutokea vizuri ama kutokea vibaya kwa uzembe tuu wa fundi........ama kwa tajiri mwenyewe kutaka kumbana fundi katika kulipia gharama, lakini anataka kitu kizuri.......
Na katika hii hii milango yetu, jamani tujitahidi mafundi wasichafue frems za milango, kwa kua kazi ya milango ni ya fundi wa rangi, basi fundi mason (fundi tope) anaichafua chafua kwa haraka zake, za kutaka kumaliza kazi mapema........ilimradi tuu... ama ana kazi nyingine sasa anataka kuziwahi sizimpite........

Huu ni uchafu wa hali ya juu, na inakuingiza wewe mwenye nyumba gharama ya kulipia kuzisafisha, maana hizi frems, zinarukia cement, etc........

Ukiangalia nyumba hizi zote hazijapigwa rangi, lakini, uchafu unatofautiana baina ya frems na frems.

Ndugu mdau nakuachia wewe ujionee na uangalie ni frems zina gani ambazo zinapendezesha nyumba ama zitapendezesha nyumba yako na kuonekana kisasa zaidi.............

No comments:

Post a Comment