Tuesday, April 16, 2013
Vyombo vya wageni.......
Hivi imeshawahi kukutokea kwamba unakwenda kumtembelea kama ndio ndugu, rafiki, etc....Halafu ukaletewa kinywaji kwenye glass ambayo inanuka mende ama harufu mbaya.....? Na kumbuka kwamba hiyo glass ilikua kwenye kabati liliko hapo dinning ama jikoni ambapo ndipo vyombo vya wageni vinapo kaaa....
Tumekua tunajisahau sana kuhusiana na hili....Hivi bado wapo baadhi yetu tunaweka vyombo kwenye makabati yetu na kusema kua hivi ni vyombo vya wageni...Yaani hata wewe mwenyewe uliyenunua haukitumii unasubiria mgeni atokeee.....
Haya basi tumekua tukichukua hatua gani ama tumejiwekea ratiba gani ya kuviosha hivi vyombo, kiasi kwamba mgeni anapotokea akipewa kitu kwenye hiyo glass isitoke harufu mbaya,
Hii ilinikutia mahali, kwamba nimekwenda, nikakaribishwa vizuri...story zikaanza, na nikakaribishwa juice, ila ile naisogeza tuu mdomoni nikasikia harufu ya mende.....(Ingekua wewe ungefanyaje)
Kwa kweli nilichofanya sikuweza kuvumilia na kumwambia mwenyeji wangu na kumpa somo....sawa alianza kwa kukasirika, ila baadae alielewa na nilichomwambia, ni kua kama umeamua kua na vyombo vya wageni, basi vyombo hivi navyo viwe vinasafishwa mara kwa mara, na kua katika mahali safi, kama vyombo vinavyotumika mara kwa mara....
Hivyo basi, nawaomba tuwe na utaratibu kwa wale tunaoweka vyombo vya wageni, tuwe tunavikumbuka kuvifanyia usafi na vyombo pia......na kabati lake pia.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment