Wednesday, April 24, 2013

Baadhi ya rangi za nje ambazo unaweza kuzipata hapa Homez Deco....Rangi za Dulux Karibuni


Ukiangalia nyumba hizi naamini hautaweza kukosa rangi unayoipenda ama hata jinsi ya kutumia rangi zaidi ya moja kwenye nyumba yako ama ofisi kwa upande wa nje.....Ule wakati wa kupaka nyumba rangi moja pekee umepitwa na wakati.......tumia rangi zaidi kwa muonekano mzuri, rangi zilizopooza.....Tuna catalogue yenye sample za rangi 3200....kwa hapa kuwezi kukosa hata kama ukija na sample yako itatengenezwa kulingana na upendavyo......





Baadhi ya nyumba ambazo tunaziona zumetumia rangi ambazo zimepooza na zikapendeza pia.......




Kwa mahitaji ya rangi za dulux wasiliana nasi, rangi hizi zinabana matumizi na zinadumu ukutani bila kupauka kwa muda wa miaka 8 tangu umepaka......




Je unaweza kutumia email kuhusiana na usafi wa nyumba zetu, Tutumie email sylvianamoyo@yahoo.com nasi tutairusha humu



Jana nilitembelewa na mdau wangu hapa ofisini kwetu, alikuja kujua suala la rangi ana nyumba yake anataka apake...so tukaongea akaona catalogue yetu ya rangi za dulux...na tukakubaliana anitumie kwa email nyumba niweze kuiona na kushauri ni rangi gani apake na nyumba iweze kupendeza..

Sasa akanikumbusha lile suala la glass niliyoletewa ikawa inanuka mende....alicheka sana, na akasema yaani umeweza kusema, kumwambia mwenyewe, nikamwambia ndio maana nisingesema ningekunywa na huo uchafu.....

Sasa tukaanza na stori za hapa na pale, akaniambia hivi jamani bado kuna watu wanatandika vitambaa kwenye makochi, hivi hii fashion si imekwisha jamani, maana ilikua ni zile enzi za mababu na mabibi zetu zama zile.....Nikamwambia ni kweli sasa hivi hii mambo ya kutandika vitambaa kwenye makochi ni kizamani ila bado tunaendelea kuelimishana......na hatimae najua iko siku watu tutaelewa na kuacha kabisaaaa...

Tukahamia kwenye swala la usafi wa nyumba....yaani hapa nilijichekea kweli, maana kwa kusema ukweli kuna tatizo...kwanza kwenye products zenyewe za usafi, na pili usafi wenyewe...utakuta mtu anafanya usafi wa nyumba yake, ila ukiangalia darini kuna buibui wametanda,.....sasa huo ni usafi kweli.....

Kwenye usafi unapaswa huanzia juu kuja chini, sasa tatizo sijui linakuaga wapi buibui zinasahaulika....ukija kwenye usafi wa chini ya makochi....na haya masofa yetu haya yanavyohifadhi panya....jamani jamani.....

Nilishakutana na sofa ambazo ndani kuna panya......yaani nilikwenda kwa client, kuangalia anataka abadilishiwe kitambaa sofa zake...na hua ninasemaga sio kila sofa inafaa, kubadilishwa, ama kufanyiwa marekebisho sasa hua ninakwenda kuangalia.....yaani jamani sasa sijui kuhusu panya nikakaa kwenye sofa baada ya kukaribishwa, tukaanza kuongea, sasa nikawa nasikia vitu vinatembea tembea....lol....

baada ya dk 3 panya huyo chini ya kochi katoka na kaingia kochi lingine....yaani acha tuuu...niliruka, maana na ujanja wangu wote panya naogopa....

Kama kawa, sikuvumilia, nikamwambia hivi unajua panya wanaletwa na uchafu ambao ndio unaowavutia....sasa haya makochi hata kabla sijaendelea kuangalia, ninakushauri uyatupe, maana tukisema turekebishe ni sawa na kununua lingine.....na utakapo leta lingine, hakikisha unatibu hili tatizo la panya, kuna dawa, na uzingatie usafi wa ndani kwako.....tukawa tumemaliza....

Matatizo kwenye nyumba kuhusu usafi ni mengi mnooo, hatutumii products nzuri za usafi, ama tuna rashia rashia tuu usafi, ama tunamwachia tuu dada afanye usafi, etc.....

Ninakaribisha kwa yeyeyote yule mwenye tips za usafi wa majumbani atutumie email ili tuweze kuelekezana humu humu kwenye blog yetu hii nami nitairusha na kusahuriana.....hakuna anaejua wote tunajifunza kupitia kwa mwingine......na kuwekana sawa

Email: sylvianamoyo@yahoo.com

Tuesday, April 23, 2013

Back yard garden designs

Landscape designs...

TICKETS ZA WOMEN IN BALANCE KITCHEN PARTY GALA ZIMEANZA KUPATIKANA.







TICKET ZA WOMEN IN BALANCE KITCHEN PARTY GALA KUPATIKANA VITUO VIFUATAVYO:
Shear illusion mliman city
Cassandra mikocheni kwa nyerere
Cassandra mjini jengo la golden jubilee floor ya kwanza
Born 2 shine Mwenge karibu na tra
Jackys cosmetics Kinondoni
Pata ticket yako mapema.


Tuesday, April 16, 2013

Vyombo vya wageni.......


Hivi imeshawahi kukutokea kwamba unakwenda kumtembelea kama ndio ndugu, rafiki, etc....Halafu ukaletewa kinywaji kwenye glass ambayo inanuka mende ama harufu mbaya.....? Na kumbuka kwamba hiyo glass ilikua kwenye kabati liliko hapo dinning ama jikoni ambapo ndipo vyombo vya wageni vinapo kaaa....


Tumekua tunajisahau sana kuhusiana na hili....Hivi bado wapo baadhi yetu tunaweka vyombo kwenye makabati yetu na kusema kua hivi ni vyombo vya wageni...Yaani hata wewe mwenyewe uliyenunua haukitumii unasubiria mgeni atokeee.....

Haya basi tumekua tukichukua hatua gani ama tumejiwekea ratiba gani ya kuviosha hivi vyombo, kiasi kwamba mgeni anapotokea akipewa kitu kwenye hiyo glass isitoke harufu mbaya,

Hii ilinikutia mahali, kwamba nimekwenda, nikakaribishwa vizuri...story zikaanza, na nikakaribishwa juice, ila ile naisogeza tuu mdomoni nikasikia harufu ya mende.....(Ingekua wewe ungefanyaje)

Kwa kweli nilichofanya sikuweza kuvumilia na kumwambia mwenyeji wangu na kumpa somo....sawa alianza kwa kukasirika, ila baadae alielewa na nilichomwambia, ni kua kama umeamua kua na vyombo vya wageni, basi vyombo hivi navyo viwe vinasafishwa mara kwa mara, na kua katika mahali safi, kama vyombo vinavyotumika mara kwa mara....

Hivyo basi, nawaomba tuwe na utaratibu kwa wale tunaoweka vyombo vya wageni, tuwe tunavikumbuka kuvifanyia usafi na vyombo pia......na kabati lake pia.

Monday, April 15, 2013

Door Mats

A door mat is a fun and affordable way to introduce your style to any front door visitor, from the mailman to your best friend. While doormats provide the valuable and essential task of keeping the mud off of your sheepskin rug, they are also a friendly and personal touch reminding visitors that someone lives inside. 


Door mats are available in a wide range of materials and colors. Door mat styles range from trench-worthy to purely decorative. Although doormats aren’t a major monetary investment, they are highly visible in your home, so it’s best to choose one that matches the amount of foot traffic you receive.








Interior and exterior door mats. Door mats made for use for either inside or outside your home are made with different materials as they are designed to handle different levels of debris. Interior mats are often thinner more uniform in texture as they are only used for cleaning minor dirt and dust off. Exterior mats serve as scrapers for your shoes, removing outside debris to protect your flooring once you step inside your home. Exterior doormats are exposed to a lot of wear and tear, so if you opt for a more decorative doormat for your front door, it will need to be replaced more often.

Decorating Colors and How to Use Them

 Orange. An often-forgotten color, orange can instantly warm up a room in even the subtlest accents. From tangerine to coral, a shade of orange can work in your home. - Contemporary Living Room by North Vancouver Interior Designer Maria Killam 
Purple. Purple isn't always the first choice for interior decorating — outside of children's spaces — but when used smartly and sparingly, it can add an elegant element of surprise to modern or traditional spaces. Contemporary Kitchen by Oakland Architect Mercedes Corbell Design + Architecture
White. Sometimes sticking to the basics is your best bet. Don't dismiss white as boring — when used right, it can make an incredible statement. Modern Bedroom by Naples Interior Designer Joie Wilson
Brown. Although beige tends to get a bad rap, there's a reason this color is so popular: It's hard to get wrong. Use a lighter shade for more soothing spaces and venture into dark chocolate browns to mix things up. 
Contemporary Family Room by San Francisco Interior Designer Mark Newman Design



Pink. Although it's a favorite choice for little girls' rooms, pink can still feel grown up and sophisticated. This cheerful hue can brighten rooms of many styles. 
Traditional Bedroom by Brooklyn Architect CWB Architects -


NB: all these colors(shades) are available at Homez Deco - Dulux Paints....

Gardening: UJUMLA KIBIHASHARA, MAKAZI YA WATU MAOFSINI NA SEHEMU NYINGINEZO



       Hata sehemu za bihashara,   zinatakiwa kuwa na mpangilio mzuri usafi, huu ndiyo mpangilio wa wenzetu, ktk dealership  zao nilivutiwa sana,  na mpangilio huo, hata  DAR   Inawezekana wenye sehemu   za bihashara mbalimbali wakaweka  mpangilio mzuri wa kuvutia.na sila zima uwe na eneo kubwa ndiyo uwe msafi la asha hata eneo dogo linaweza kuvutia nakuwa safi.










Kitchen Party Gala 2013




Fixit SmoothOver Skimming Plaster for Exterior & Interior walls..... available at Homez Deco......




An easy way to give a perfectly smooth weatherproof finish to rough or uneven plaster. Ready mixed for easy use, it will skim up to 5m thick and is specially formulated to adhere strongly to plaster. Simply skim it on and smooth it off, it will set hard in 4 hours to a white, weatherproof and alkali resistant finish that does not need to be primed before painting.

1. Stir to a creamy consistency.


2. Apply Fixit SmoothOver with a wet plastering trowel, skimming tool or large scraper moving in an upward curve maintaining a firm and even pressure. Applying only as much Fixit SmoothOver as needed, it is advisable to build the film thickness in multiple layers rather than one thick coat (maximum thickness 5mm). Don't worry about small irregularities or "tramlines".


3. Allow to dry for at least 2 hours before sanding with 100Gritt sand paper to a smooth finish. Thick applications or damp weather may require a slightly longer drying period.


4. As an alternative to sanding, Fixit SmoothOver can be floated or polished. As soon as Fixit SmoothOver is dry enough to touch (not fully dry), use a wet foam trowel to polish the surface in a circular movement, cleaning and wetting the trowel beween strokes to achieve the ultimate Fixit SmoothOver finish.


5. After 6 hours you can overcoat with any Dulux® water based paint. Allow to dry for at least 16 hours before overcoating with Dulux® enamel paints.


6. You do not need to prime before painting.


NB: Instead of using gypsum powder on your walls this is a right product for your walls....

Storage
Do not use or store in extremes of temperature and protect from frost.

Available in the following sizes
1.5Kg, 20 Kg

Cautions
Please read instructions.


Prices:
1.5 kg = Tshs 10,030.

20 kg = Tshs 



Sunday, April 7, 2013

Sio wallpaper, ni urembo wa ukutani.......

 Nilikwenda kwenye nyumba moja hivii huko mbezi ya kimara kupima curtain rods........na nikakutana na hii decoration ya ukutani......hii ni aina rangi ambayo inapakwa kwa kutumia spongi maalumu, na ina rangi yake maalumu kwa urembo huu kutokea.......imependeza kwa kweli....Hapa alitumia brown kwenye korido ya kuingilia ndani......
 Na kwenye korido alitumia nyeupe.....

Hivi ndio inavyoonekana kwa karibu.......

Asante mteja wangu kwa kunielekeza ni wapi urembo huu unapatinaka.......nitawatembelea na nitawaletea humu humu na maelezo yoteee........