Monday, February 25, 2013

Kitchen Hood.....

Hili ni jiko la mdau wetu.....ambapo Homez Deco tulimpakia rangi za Dulux...Lakini pia nilivutiwa na jiko lake.  Mnakumbuka kuna siku katika blog yetu nilizungumzia kuhusu Kitchen Hood, na kazi yake.....Kazi yake ni kunyonya unyevu na mvuke ambao hua unachafua sana jiko.....
Nilipendezewa pia na jinsi alivyo weka lebo katika kontena zake za kuhifadhia chakula...Kama inavyoonekana hapa.....Hata siku moja haitaweza kukupa shida ya kuanza kutafuta kontena ipi ina nini.......maana unaweza ukawa una kontena nyingi na zikakuchanganya...

Hili pia nililizungumzia la kuweka lebo kontena za chakula. na zinatakiwa ziwe zinazoonyesha ndani kuna nini.....
Mimi binafsi nilipendezewa na jiko lake,

Napenda kuchukua fursa hii kukupongeza mdau wetu, kwa kua na jiko zuri na safi na lakisasa.....

(nitaomba contacts za hawa waliotengeneza jiko hili ili wadau nao muweze kua na majiko ya kisasa kama hili, maana finishing yao ni nzuri mno)

Nitalipiga picha jiko zima na kuweza kuwaletea humu humu.......

1 comment:

  1. A kitchen hood b is an essential kitchen appliance that helps remove smoke, steam, grease, and cooking odors, keeping your kitchen air fresh and clean. When searching for kitchen hood price in Pakistan, you’ll find a variety of models and brands available at different price ranges to suit different budgets and kitchen sizes. Quality kitchen hoods not only improve ventilation but also add a stylish touch to your cooking space.

    ReplyDelete