Monday, January 21, 2013

Unahifadhi wapi products zako za bafuni, bafuni kwako?



 Hizi ni baadhi ya design za mabafu, ambapo zinatuelekeza ni vipi tuweze kuhifadhi products zetu kwa usalama na usafi zaidi....na katika mpangilio mzuri... hakikisha pia bafuni kuna kaa pakavu muda wote, nirahisi mno, mtu anaenda kuoga ahakikishe anakausha maji, kuanzia ukutani, mpaka chini. hii itasaidia sana kuhakikisha kua panakaa pakavu..

 Mpangilio mzuri, usafi ndio unaohitajika katika bafu lako...weka products zako kulingana na ukubwa wa sehemu ya kuhifadhia....
 Hii ni design nzuri pia ya kuanika mataulo...hii ni miti iliyofungwa vizuri, na itayarishwa vizuri, ili iweze kutumika kwa ajili ya kuatundikia mataulo.....(fundi wa mbao wa hapo jirani nawe anaweza kukutengenezea ukihitaji na kama umependezewa nayo....)
 Bafu hili ni kubwa, na hata unaona storage yake ni kubwa, ukiangalia juu, na kabati za chini....zote hizo ni sehemu ya kuhifadhi vitu vyako vya bafuni......



 Design ziko nyingi, ninaamini huwezi kukosa moja kwa ajili ya bafu lako.....

 Design hizi hapo juu ni ubunifu kidogo tuuu. na ona inavyopendeza, na waweza kupaka rangi yoyote upendayo na ikapendeza....


Haijalishi ni rangi gani unapenda kupaka kwenye bafu lako, ila jitahidi ziendane na accessories za bafuni,
Bafuni si mahali pa kupadharau na kupaacha pachafu, kisa ni sehemu ya kuoga.....hakikisha usafi wa bafu lako unaupa kipaumbele, maana magonjwa yataanzia hapo hapo bafuni, na kuenea sehemu zote....

Products za usafi ziko na nzuri tena za kila aina, na zenye harufu nzuri....

No comments:

Post a Comment