Monday, July 30, 2012

Njia 18 za matumizi ya vikapu.....

 Habari zenu ndungu wadau.... Leo nimependa tuongelee juu ya matumizi ya vikapu, kwa upande wa kuhifadhi vitu.....Vikapu ni vizuri sana kwa ajili ya kuhifadhi vitu, na vina matundu, matundu ambayo hupitisha hewa... picha ya kwanza hapo juu inatuonyesha kua, vikapu vyaweza kutumia kwenye makabati,, na pia ukaweka label ya majina ya wanafamilia yako, kwamba wasichanganye....
 Picha hii ya pili hapo juu, ni kapu hilo sie huku hua tunatumia sana kwa kwendea sokoni... lakini pia linaweza kutumika kwa kuhifadhiwa vitu, na ukisha maliza kulitumia kwa muda huo, basi lirudishe na ulihifadhi kwa usafi mahala ulipoamua liwekwe.....waweza kutumia kwa kuweka vitabu, magazeti etc,
 Bafuni pia hakujaachwa nyumba.... vikapu hivi hufaa sana na hupendeza sanaaa huku bafuni, ni wewe tuu kuamua unawekea nini, na sehemu utakayoiweka pawe panaukubwa wa hilo kapu kuingia, na kwa mpangilio ulio mzuri.

 Haya chini ya kiti pia waweza weka, kiti hiki kimetumika kama kiti, na kama stoo, maana kuna droo, na kuna kapu chini yake, 3 in 1.......nyumba zisizo na nafasi, hii kwao ni nzuri zaidi....
 Chini ya meza pia waweza weka vikapu, na kukapendeza pia.... hupunguza sana vitu kukaa ovyo ovyo....
 Vyooni napo kapu hutumika,, kwa kuwekea mataulo, nguo chafu etc... ni wewe tu upange uwekee nini, ila chooni kusiwe na maji maji sasa.....

 Jikoni, mpangilio huu hupendeza sana.....na kufanya jiko lako kua safi.....


 picha 3 hapo juu, kapu zimetumika kwa kuhifadhia vitabu, files kwa ofisi za majumbani......
 waweza kuweka chini ya uvungu makapu kwa kuhifadhi mashuka, etc.... lakini kwa uhifadhi wa chini ya kitanda, inabidi uwe makini sana, maana waweza kusahau kutoa ili vipate hewa, maaa ukajaza sana mavitu chini ya uvungu na kukuletea harufu mbaya ya uvundo, na hata wadudu, sasa tuwe makini katika hili....
 Jikoni pia mpangilio wa makapu hupendeza....
 Makapu kwa kuhifadhi vitu visivyotumika mara kwa mara ...
 makapu yenye divider, inapendeza kwa kweli....

kwenye kabati za jikoni.... hutumika pia na kuleta mvuto.. na muonekano mzuri.....

Nawatakia mwanzo wa wiki mwema......

No comments:

Post a Comment