Wednesday, June 27, 2012
Uzinduzi wa Rangi za Dulux za kampuni ya Sadolin Paints..
Nilipata picha ya pamoja Kutoka Kushoto, Vailet, Mimi, Mr. Geoffrey yeye ni Protective Coating Manager, na Renalda, tukiwa na zawadi zetu.......
Ukuta umepigwa rangi na tuliohudhuria.......
Nilialikwa na Mr. Ilyas, yeye ni Sales Manager .........
Mlango ulipigwa vanish........
Nilivyoona hii picha kwa kusema ukweli, nilimkumbuka Jaydan wangu, enzi hizo.... tutakavyokimbizana kwa utundu.... hahahhahha hahhahha..... hahhahah
Rangi za milango/mbao zipo pia........unang'aa mlangooooo kama kioo..........hahhahahah nice.....
Kulikua na fashion show ya watoto walituandalia.....
Nilipenda huu mchoro..........
Kuta zao kwa nje ya madarasa, wamechora picha za Tinga Tinga.... zinavutia sana,......si unaona ni kama wamebandika... kwa jinsi zilivyopendeza......
Huu mti sio wallpaper, umechorwa kutumia rangi zao, na umependeza kweli.... hongera kwa mchoraji.....kwa kazi nzuri....
Tulipata fursa ya kupaka rangi kwenye moja ya kuta waliyotuandalia..... na watoto......
Ilikua ni jumamosi ya wiki iliyokwisha, nilialikwa kwenye uzinduzi huu, na siku ilipofika nikawasili hapo. Shughuli ilifanyika katika kituo cha kulelea watoto cha SOS.....
Rangi hizo mnazoziona nje ya majengo ndizo za DULUX za kampuni ya SADOLIN Paints.... najua wengi wetu tunaifahamu kampuni hii ya Sadolin...
Uzinduzi wa rangi hizi mgeni rasmi alikua Mheshimiwa mama Salma Kikwete. Mheshimiwa mama Mary Nagu pia alikuwepo, na wengineo....
Shughuli ilikua nzuri, na ilienda vizuri, na tulipewa nafasi ya kujaribu rangi hizo kupaka ukutani na kujionea wenyewe...
Kwa kusema ukweli rangi hizi za DULUX ni nzuri, na ziko rangi za kila aina unazozitaka, kutokea kwenye rangi zilizo pooza, mpaka zile kali.....(from neutral colors, cool colors, warm colors etc.....)
Ninapenda kuchukua fursa hii kwa kushukuru kualikwa na kujionea mwenyewe..... na nimealikwa kiwandani, kwenda kujua zaidi ya hizi rangi, na kupata maelezo zaidi juu yake..
Ninawaahidi kuwaletea yote nitakayokua nimeyapata kutoka kwao...........
Bila kusahau nilipewa zawadi......... unataka kujua ni zawadi gani hiyooooo.......
Endelea kua nasi......
NB:
Niliwaahidi mwaka huu na kuendelea, mungu akitupa uhai, nitawaletea vitu vizuri, vya kuboresha ujenzi wa nyumba/ofisi zetu....... na kuremba nyumba kisasa.........Kazi imeanza sasa..........
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment