Friday, December 21, 2012

Rangi zilizotumika katika kila chumba......




















Kwa mtazamo wa umakini, hapa utaona katika kila picha rangi zilizotumika na zilivyotumika.......kwani hata wewe zitakusaidia kuzitumia nyumbani kwako ama ofisini kwako...

Nawatakia maandalizi mema ya sikukuu ya X-mass

Napenda kuchukua fursa hii kuwa takia sikukuu njema......najua weekend hii watu mtakua busy na maandalizi ya hapa na pale....

Nasi pia tunaelekea kumalizia kufanya delivery za wale wote waliotoa oda.....kwetu....

Nitakua busy, ndio maana nimeona niwatakie sikukuu njema mapema....msije mkashangaa imekuaje.....hahhahah.....

Wishing you all Merry X-mass........


Thursday, December 20, 2012

Color of the year 2013....Pantone 17-5641 Emerald








Hii ndio rangi ya mwakani ya 2013......tutaendelea kuiangalia ni jinsi gani tunaweza kuitumia kwenye nyumba zetu, maofisi etc......endelea kua nasi.....

Siku zimekaribia za X-mass......

Nimekua kimya kwa siku kadhaa, na hii ni kutokana na kukimbizana na muda kwa ajili ya kumalizia oda za wateja ambazo wameoda kwa ajili ya sikukuu hizi......

Nashukuru mungu mpaka sasa, ni 90% kazi imefanyika na zimewafikia wateja,,,,

Naomba mniwie radhi kwa kua ilikua ni mchaka mchaka, na picha sikuweza kuchukua....

Nawatakia siku njema.....

Sunday, December 9, 2012

Mapambo ya milangoni....zinaitwa wreath......





Mapambo haya ya milangoni katika kipindi hiki cha sikukuu, yanapendezesha sana nyumba.....maana utakuta nyumba kwa nje imepooza lakini ukiingia ndani ndio unakuta kuna mapambo....

Pamba nyumba yako kuanzia nje mpaka ndani......hizi ni baadhi tuu yaa mapambo...waweza buni mapambo yako na yakapendeza sana.....

Tumejiandaaje na sikukuu....ya Xmass na Mwaka mpya....






Hizi ni baadhi ya mapambo, katika sikukuu ya xmass na mwaka mpya hua tunapamba, haijalishi nyumba ni kubwa ama ni ndogo,,,unachotakiwa ni kupamba kulingana na ukubwa wa nyumba yako,,,,hizi ni baadhi ya picha ambapo unaweza jionea kwa jinsi zilivyopambwa.....

Kuna miti ya xmass, mito, kuna zawadi zinazokaa chini ya miti.....na mapambo mengine....

Friday, December 7, 2012

More wallpapers......




Nimepata maswali kuhusu wallpapers, kama zinaharibu ukuta ama la...Jibu ni kua haziharibu ukuta na zinakaamuda mrefu ukutani.....

Tuna kuja kukubandikia, na hauna haja ya kununua gundi kwa bei ya tofauti......Bei ya wallpapers ni kwa  square meter 1 = 30,000/- sasa inategemea na ukuta wako zinaingia roll ngapi kulingana na vipimo vya upana na urefu...

Unachotakiwa ni kunitumia vipimo vya ukuta yaani upana na urefu. halafu nitakuambia zinaingia rolls ngapi.

Kubandika wallpapers ni ukuta mmoja ambao wewe utaupenda, kwa mfani kwa sitting room tunabandika ukuta ambao ni wa tv.....

Kuta zenye madirisha wallpapers hazikai vizuri..nikiwa na maana hazina mvuto mzuri.....

Karibuni sana kwa mahitaji yako ya wallpapers...

Nawatakia maandalizi mema ya sikukuu....

NB: Wallpapers zinatoka USA na UK....

Tuesday, December 4, 2012

CHUMBA KIMOJA MUONEKANO TOFAUTI.....

Rangi hufanya chumba kuonekana kikubwa ama kidogo, hii ni dinning room kama inavyoonekana, na rangi zilizotumika hapa ni dark colors, ambapo zimefanya chumba kuonekana kidogo na kina giza.......
Hapa dinning room, ile ile imepakwa rangi ambazo ni light, ambazo unaona kua chumba hakina giza na kinaakisi mwanga kwa kiurahisi na nafasi pia inaonekana ni kubwa.....

Hivi ndivyo rangi zinaweza kufanya chumba ama nyumba yako kuonekana, kama unataka nyumba ama chumba kiwe kina muonekano mdogo, basi paka rangi za dark colors, na kama unataka chumba kionekane kidogo paka rangi light colors, na waweza kuchanganya rangi, yaani ukuta mmoja ukawa na rangi ingine tofauti na za kuta zingine....

Karibu Homez Deco kwa mahitaji yako ya rangi kutoka Sadolin paints, rangi za Dulux. Tutakuja nyumbani kwako kukupa mahesabu ya rangi kiasi gani zinatakiwa, na utachagua kutoka kwenye color sample ambazo ziko rangi/shades zaidi ya 2000.....

DELIVERY OF WALL PAINTINGS (DULUX PAINTS) FROM SADOLIN


 Gari la Sadolin Paints kama linavyoonekana likiwa limewasili ofisini kwetu, Homez Deco Kinondoni....




Nikiwa nakabidhiwa rangi, na nikikagua rangi ambazo nilitoa order kutoka kwao......Hizi ni rangi za dulux, zimeshaanza kununuliwa na wateja wamezikubali, kwa kubana matumizi ya rangi nyingi, na hudumu zaidi ya kuanzia miaka 8-10 baada ya kupaka, na bila kupauka.....

Kwa wale wenye kuta ambazo zinasumbuliwa na ukungu, ama fangasi ya ukuta, sehemu zenye maji maji....ipo product ya kumaliza tatizo hilo......

Karibuni sana.....

SOFA, BEFORE AND AFTER......(maandalizi ya X-MASS hayo.....wewe umejiandaaje)



 Sitting room ikiwatayari imebadilika.....Homez Deco tuliweza kuibadilisha sofa kidogo iweze kupata muonekano mwingine.....tuliweka foronya za green, cream na animal print.....Color ya sofa ni dark brown.....
Hapa sofa ikiwa bado haijabadilika muonekano.....