Thursday, November 22, 2012

Site ya Kitunda (Dar) - Homez Deco, tuliweka curtain poles, pazia na vitanda vya chuma na neti .....


 Hapa ndio sitting room baada ya kazi kumalizika jinsi kunavyoonekana...rangi ya ukuta ni blue....hivyo nikaweka pazia hizi, zenye doti doti ziweze kuleta mvuto zaidi.....


Kitanda .....kikiwa na neti yake....(ijulikane kua hatuuzi kitanda na godoro)
 Dinning room pazia zikiwekwa vizuri...
 Dinning room
 Pazia za dinning room
 Pazia za chumbani.....
 Sitting room,
 Pazia zikiwekwa vizuri za sitting room
Hizo ni pazia za jikoni, na hizo nyaya ni za hita......

Nina tatizo kidogo la network, ila linafanyiwa kazi.....Nitawaletea picha zaidi, tukisha solve tatizo hili.....

Nyumba hii  ni mpya, na mwenye nyumba anataka kuhamia mwezi wa kumi na mbili, hivyo anafanya kwa awamu, tumemaliza pazia, vitanda, sasa anajiandaa kuweka furniture zingine zilizobaki, kama sofas, etc.......

Tunaomba radhi kwa usumbufu uliojitokeza......

Wednesday, November 21, 2012

Sorry kua kimya...

Napenda kuwaomba radhi kwa ukimya wangu....Nilikua ninauguliwa na mtoto. na pia naomba kwa baadhi ya wadau, msiwe mnanilaumu, mkiona kimya mjue kuna kitu siwezi kaa kimya bila ku update blog, nami ni binadamu na matatizo humtokea kila mmoja wetu......

Samahani kwa usumbufu mlioupata....

Wednesday, November 14, 2012

I love my self......



Ukijipenda kwanza wewe mwenyewe, basi hata wengine watakupenda. haijalishi una hali gani, tariji, maskini,    mnene ama mwambamba, mfupi ama mrefu, jikubali kwanza wewe mwenyewe na ridhika ulicho nacho......

Kwa kweli ninajipenda mimi kama mimi, na ninafurahi kua mimi kama mimi, na ninafurahia mafanikio yangu mpaka hapa nilipo tena kwa juhudi zangu binafsi.......napenda kazi yangu na ninajivunia kwa kazi yangu...kwani ndio iniwekayo mjini......

Kwa upande wa ngozi yangu hakuna mkorogo hapo hata kidogo.....ni products za shear butter ambazo ziko njiani zaja toka marekani......nitawajulisha humu humu zikifika.

Napenda kushukuru wateja wangu wotee kwa kuni support, na kuniamini, etc.......yaani sijui hata nisemeje.....ninawashukuru mno...

Kazi inaendelea kama kawaida......na tukumbuke ndio tunaingia mwezi wa kumi na mbili...sikukuu ndio hizo karibu....tumejiandaaje?

Kwa upande wa pazia, rangi za ukuta, kubadilisha vitambaa sofa, mapambo, mpangilio wa nyumba, vitanda vya chuma......etc.

Haujachelewa kabisa......Karibu tuwasiliane kwa mahitaji yako ya nyumba yako.