Thursday, June 14, 2012

Rangi za ndani za nyumba zetu........








Hili somo nimekua nikiliongelea kila mara..... na naomba mniwie radhi kama nitakua ninawaboa, ninasema hivyo kwa sababu, hili limekua ni tatizo kubwa kwetu, na nimekua nikilishuhudia katika kazi zangu huko niendako......
Nimeweka hapa baadhi ya charts ili mjionee ni jinsi gani ya kutumia rangi hizi ndani ya nyumba..... kama unataka kutumia rangi kali basi changanya na zilizopooza na zinazoendana, na zisiwe ni za giza....
Katika interior design, epuka kupaka ama kutumia rangi za giza, maana zinafanya nyumba inakua ni giza, ndogo, etc....
Mfano:
Waweza tumia rangi 3 kwa wale ambao wanapenda kuremba nyumba bila kutumia wataalam,, hii itakusaidia usijichanganye.
kwanza, unatakiwa kujua unapendelea nini? na unataka nyumba yako iwe na mandhali gani, kama ni ya misitu, bahari, etc......basi nenda na rangi hizo.... kama ni misitu basi tunajua kabisa rangi yake ni kijani, kama ni bahari rangi inakua ni ya sky, blue......
Hizi rangi ndio zinakua ni main color zako, yaani waweza zipaka ukutani, kinachofuatia, tafuta rangi inayoendana ya pili ambayo haita kua kali.. na hii ukaiweza kuitumia kwenye sakafu, carpet, tiles, etc...
Na mwisho, hiyo rangi ya tatu, itumie kwenye mapambo, pazia, viti etc...
na hapo utakua umemaliza ku pamba nyumba yako kama mtaalamu.....

Wengi wetu tumekua tukifanya makosa ya kutumia rangi nyingi bila mpangilio mzuri.... angalia baadhi ya picha hapo juu najua itakua imekupa mwangaza wa nini ufanye ili kuepuka makosa hayo....
Somo hili nitakua nikiliongelea mara kwa mara naomba tusichokane......
kwa maswali karibuni......

sylvia
Director....


Round About near Hindumandal Hospital.... Dar




Jana kwenye mizunguko yangu, nilipita maeneo haya, kwa kweli nilivutiwa sana na mazingira ya hapa..... Kweli Dar tukiamua tunaweza...

Ubunifu huu niliupenda sana hasa ukuzingatia kua Dar maji ni shida, sasa kwa waiobuni hivi nawapa hongera sana...

Hayo mawe yanatokea hapa hapa kwetu Tanzania. yako Morogoro....


Hongereni sana Kwa wahusika........



Tuesday, June 12, 2012

Homez Deco - Kreative Homez....... Kazi yetu.... Site ilikua kigamboni.....


Haya nikiwa kwenye kazi yangu, kwa furaha sana sana.... asante mteja wangu kwa kufurahia kazi yangu......Tunaleta mpaka nyumbani...... Karibuni.....

Dressing table......

Fundi akitayarisha vioo, vya kuweka kwenye dressing table na side table...... yaani kitanda kilipendeza sana, sijisifii ili nyumba ilipendeza,


Hiki ni four poster, kitanda

Chaga zikiwekwa, wengi wamekua wakiuliza chaga zinakua ni zipi? jibu ni kua, chaga ni za mbao, nani imara sana vitanda hivi, ......
Mafundi wakifunga vitanda...