Homez deco tuliweka curtain poles.... vyumbani, nilipenda na vingine.....
Nilipenda design ya makabati ya jikoni, na jiko lake ni dogo, lakini ameli design na limependeza sana... simple and neat.........top ya makabati ni marble.... hapa wengi tunachanganya sana kati ya marble na formaica,
Ninashauri kwa jikoni, tutumie mbao, makabati na top ziwe ni marble.... maana sikuhizi kuna hizi mdf, zinazotengenezea makabati, jamani zile hazitaki maji kabisaaaaaa... sasa ukiweka jikoni na jikoni kuna maji,,,, utakuja kuniambia.....na mbao nchini kwetu tunazo, na mafundi wako, na nitajitahidi kuwaletea contact za mafundi pindi ninapopata, na kuona kazi zao nikaridhika nazo,
Niipenda pia nyumba kwa nje... nyumba haijahamiwa bado, na ni juu na chini, yaani ni familia mbili watakaa hapa..... Nzuri sana na imependeza.....hii design ya madirisha kwa nje, naona ndio iko kwenye fashion sasa, nyumba nyingi inazo, na inavutia....
Hii ni corridor, nilipenda hizo nguzo, natafuta contacts zao nitawapa, soon,
Bafu....
Toilet..... Tiles ziko nyingi na za aina tofauti, na ubora tofauti, sasa ni wewe tuu chaguo lako , na jinsi ya kuzipangilia ziweze kuendana, nzuri sana.....
Kwa haraka tuu nilivyoingia ndani ya hii nyumba nilijua tuu mwenye hii nyumba anapenda sana neutral colors......
Nashukuru sana kwa mwenye nyumba kwa kunipa ruhusa na contacts za mafundi ili sisi sote tuweze kupendezesha nyumba zetu,
Na ninaamini kwa kufanya hivi, mafundi feki watajichuja tu wenyewe.....
Namba ya fundi ni 0753-218817
NB:
Mafundi hawa, sijaonana nao, ingawa ninatafuta muda nionane nao, niendapo site, nikipendezewa na kazi zao basi ndio ninaomba contacts, kwa wenye nyumba..... Ninawashukuru wote wenye nyumba kwa ushirikiano wao.....na tuendelee na moyo huu wa upendo..........
Tuesday, June 26, 2012
Wednesday, June 20, 2012
Site ya Kigamboni....
Sink kama linavyoonekana hapa juuu...napenda kushauri kua kwenye sinks, muweke kabati, kwani inakusaidia sana kuhifadhi vitu vya bafuni na kukaonekana kusafi muda wote, vitu kama toiet paper, sabuni za vyooni etc....
Bafu hiloooooo....
Jiko nalo haliko nyuma kabisaaa.....unajua ukijiamini n kujua unapenda nini, na kufuatilia majarida mbali mbali, ama kwenye mitandao, basi unaweza...decorate nyumba yako na ikapendeza.... pia....wenye nyumba hawa waliamua kusafiri wenyewe, kufuata mzigo, yaani kuanzia, grill, miango, jiko, tiles etc, china na wanasema waliokoa pesa kwa kiasi kikubwa tuuu.....
Hii ndio nguzo ilivyonakshiwa......na nilichopenda, layer yake ni kubwa, yaani hawajabania kabisaaa........
Hii ukutani sio tiles, ni design ambayo wataalamu wanachanganya ndio wanaweka ukutani, ukiingalia kwa karibu, ni kama undongo hivi.......imekaa vizuri kweli yaani....
Nilivutiwa na nyumba hii nilivyofika, kwani ukiangalia ukuta kwa nje umependeza, kwa design yake, ukiangalia kwa taratibu utaona jinsi nguzo zilivyonakshiwa......
kwa watakaohitaji huduma hii ninawaletea contacts zake kesho mapema......
Hongereni sana wenye nyumba, na ninashukuru sana kwa kunikubalia kupiga picha na kuja kushare na wadau wenzetu, ili wajue ni wapi wapate vitu vizuri...
NB:
Ninawaomba wadau wote kua kama unajua kuna mahali vitu vinapatikana vya majumbani, iwe ni mapambo, vitu vya ujenzi, naomba usisite kuniambia, unipe contacts zao halafu nitawatafuta na kuwasiliana nao, na kuwaletea nini wanafanya, na ninaomba ushirikiano wenu ninapoomba kupiga picha nyumba zenu, ili kuja kushirikiana na wadau wenzetu, naomba mnikubalie, kwani sitotaja majina ya mwenye nyumba, ama details zozote zitakazofanya kujulikana kua nyumba hiyo ni ya nani kwa upande wetu....ninajitolea kufanya kazi hii bila malipo yoyote.
Asanteni sana, na mungu awabariki.....
Tuesday, June 19, 2012
Kabati za ndani.... Mbao aina ya mninga....mbao zetu....
Jumapili ya juzi, nilikwenda site eneo la Goba....., lengo ni kwenda kupima pazia, na hii ni baada ya sisi kuweka curtain poles, kama kawaida yangu, jamani kizuri kisifie.....na chema chajiuza....
Nyumba hii ni nzuri, na nilipenda na nikamsifia sana mwenye nyumba, na ninapenda kutoa shukrani zangu za dhati kwa kuniruhusu kupiga picha ili tuweze kushirikiana katika hili...
kuna msemo usemao, kizuri kula na nduguyo, na kibaya ........
Nilipenda kila kitu, yaani tiles, makabati etc.....
Nimeonelea tuangalie makabati haya na uniambie kua umeyaonaje,
kwa mtazamo wangu, fundi aliyeyatengeneza haya makabati anastahili sifa, maana haku chakachua, na finnishing yake ni nzuri. maana hata milango pia ni mninga......na fundi huyu hana usumbufu wa kazi.......
kwa mahitaji ya milango makabati wasiliana na fundi huyu
anaitwa fundi Dennis - 0715 - 888680
Ninamshukuru tena mteja wangu huyu kwa kutupa mawasiliano ya huyu fundi ili wote tusingie hasara, maana mafundi asilimia kubwa ni kula hela za watu na kiswahili kingi....
Subscribe to:
Posts (Atom)