Thursday, May 8, 2014
USAFI WA MILANGO YA MBELE YA NYUMBA ZETU.
Asilimia kubwa ya nyumba za Kitanzania milango ya mbele ya nyumba zetu hua hatuitumii....yaani labda mgeni kaja...au labda tunataka kuiniza vitu ndani ndio tunatumia huo mlango.
Asilimia kubwa hua tu atumia mlango wa nyuma ambao ni wa jikoni...
Sasa basi naomba tukumbushane swala la usafi wa mlango wa mbele...hata kama hauutumii jamani mlango huu unahitaji kua msafi muda wote...
Unapofanya usafi sitting room fungua na mlango huo ufanye usafi pia...
Haileti maana eti mlango unafanyiwa usafi mara chache kisa hautumiki ama mpaka mgeni aje au unataka kuingiza vitu ndio ufanyiwe usafi.
Nyumba inatakiwa kua safi muda wote...wakati wowote...kwa afya yetu na kwa muonekano safi....tuwe tunawakumbusha na kukagua wadada wa kazi ama wasaidizi wetu na maramojamoja uwe unatokea mlango wa mbele hii itakusaidia kukagua na kujenga mazoea ya kufanya usafi eneo hili.
Wednesday, May 7, 2014
SHADES OF YELLOWS. ......
Rangi ya njano....ikitumika vizuri huleta mvuto na hupendeza.......na kwa sababu rangi hii ni kali basi inashauriwa kutumika kidogo...sehemu ambapo unataka itumike....
Rangi hii ya njano....inaweza ikawa imeiva...imepauka....imekolea....maana katika rangi moja inaaminika hua inabadilika mara 24...kuanzia ikiwa imeikolea mpaka kupauka...sasa inategemea na matumizi yako na wapi unataka kuweka.
Rangi hii inaweza kutumika katika mapambo...ofisini...majumbani ...etc...ili mradi tuu ipangiliwe vizuri.....
Rangi ya njano...inaweza kutumika...chumbani kama kwenye mapambo....na iliyopooza ukutani...ama sebuleni.....kwenye mapambo pia..ama jikoni....ukutani ama vyombo ama jiko lenyewe....vyooni pia....basi ilimradi tuu itumike kwa uangalifu...mkubwa isije ikakukera...baada ya muda mfupi.
Sunday, May 4, 2014
AC KWENYE NYUMBA ZETU.
Ndugu wadau....hua najiuliza sana na sipati jibu..ya kwa nini kwenye nyumba zetu ile sehemu yenye AC kwa chini yake hua tunapaacha wazi hatuweki hata picha ....maana hua panaonekana pako wazi mno....
Ingawa inategemea na AC yako ulivyoiweka....
Nivema kuweka AC na ikawa na muonekano mazuri....na wa kuvutia....shautiana na fundi usimwachie ajiwekee ilimradi kaweka...
Thursday, May 1, 2014
KITI HIKI NI CHA SALOON.......HARD WOOD..
kwa wezetu wa nchi za nje viti hivi hutumika kukalia directors wa movies.....ila sie tumeweka kwa matumizi ya saloon na bado inamedeza pia...
Kiti hiki koko comfortable. ...na ona inavyopendeza.....emagine uko saloon...then umekaa kwenye kiti hiki...
wasiliana nasi kwa uhitaji wa hard wood....furniture aina yoyote ile...iwe ni catalogue yetu ama yako....njoo nayo tuta discuss.....0713-920565.
HARD WOOD. ...LOVE CHAIR.....
Kinaweza kuwekwa kwenye balcony yako...ama sitting room...ama kwenye gazebo....vile vinyumba vidogo vya vya kupumzika....vya nje....
orange imetumika kuongeza kionjo cha kochi hilo....maana rangi za mito mikubwa zimepooza...ila tulipoweka orange hapo kidogo..kochi limeonekana.....
Subscribe to:
Posts (Atom)