Naomba niwafahamishe wadau wote kua, kabla ya kufanya design ni lazima tujue kua jiko hili litatumikaje? na eneo letu litatutosha? kuna aina mbili hapa, kuna jiko ambalo tayari limesha jengwa, na kuna lingine ambalo bado halijajengwa.
Kwa hili ambalo limejengwa tunachokifanya ni kucheza na space iliyoko katika ku design........
Ambalo halijajengwa tutaanza maandalizi, na kidogo hii hua nirahisi zaidi, ambapo tunahitajika kujua ni watu wangapi watahitajika kuwepo katika jiko letu, na je watapishana vizuri, na je nafasi itahitajika kiasi gani kwa ajili ya makabati, jiko, sink, fridge etc....
Nakumbuka kipindi cha nyuma nilishawahi kuzungumzia aina za majiko, na utachagua jiko lako liweje kulingana na ukubwa wa eneo lako la kiwanja. na hata kama limesha jengwa basi itaaangaliwa ni design gani inaweza kufaa kwa jiko lako, na kama kutakua na marekebisho madogo madogo basi yatafanyika ili kuweza kuwekwa sawa.
Kuna ile tabia ya kulazimisha kuweka vitu vikubwa wakati jiko lako ni dogo. ama vitu vidogo wakati jiko kubwa. vitu viwekwe kulingana na eneo. Ninaongelea utakuta jiko dogo lakini mtu kaweka double door fridge.....ama jiko la plate 6, ama double sink....haya ni makosa...
Napenda kusema kua kabla ya kuanza ujenzi, jitahidi ujue kila sehemu itatumikaje, na kwa ukubwa gani.....watu wa design watakusaidia katika kuchanganua ama umwambie nini unataka hata kama ni vingi, halafu vitachambuliwa na kufanyiwa kazi.
Aina za jiko ni:
L-shape
U-shape
Gallery -shape
Straight line- shape
(nitarudia tena somo hili la aina za jiko)
Siku hizi naona baadhi ya nyumba tiles zinawekwa mpaka juu. napenda kuwaambia kua sio lazima, unaweza kuweka tiles katikati ya makabati ya juu na chini na kukapendeza mno. sehemu inayobaki ikapigwa rangi.
Kwa kwenye ku fanya fittings za makabati, utakuta nyumba nyingi tunaacha nafasi kubwa kutoka kwenye cyling mpaka kabati inapoanzia. Hilo ni kosa....maana ile nafasi inaweza kutumika. yaani hizo kabati zinakuwa ni ndefu, halafu kule juu unaweza kuweka vyombo vyako, vitu vyako aambavyo huvitumii, na vinakaa kiusafi maana vinakaa ndani ya makabati, na sio kukaa juu na kuonekana mlundikano wa mavyombo etc...
Sasa basi unaweza kuweka milango ya kabati ikiwa ni mbao mwanzo mwisho, ama milango inakwa na vioo.....uzuri wa kua na vioo kwenye milango, ni kua hautohangaiika kutafuta chombo unachohitaji, maana utakua unakiona kabla haujafungua kabati. na utakua unavipanga mara kwa mara maana utakua unaona kama vimevurugika katika upangaji wake. na siku hizi unaweza kuweka taa kwa ndani kuweza kuona vizuri, na kuleta muonekano mzuri katika makabati haya.
Kwa upande wa madirisha ya jikoni. yasishuke chini sana ama kua juu sana. maana sink mara nyingi hukaachini ya dirisha, kwa kua outlets zake hutoka nje......na sink nalo sisikae juu sana mtu mpaka kuosha vyombo inakua ni vigumu.
Finnishing nayo inahusu sana hapa....je milango iweje ya kabati, vanish, sakafu, madirisha yaweje, pazia etc.....je utatumia mbao ama makabati ambayo ni ready made....yote hii ni kulingana na mfuko wa mteja.
Kila kitu kinakwenda kwa vipimo katika nyumba........hakuna kitu kinaitwa kukosea.....ni bora ujenziukafanyika taratibu kwa umakini na ufasaha, kuliko haraka haraka, ndio tunakoanza kulipua kazi.......naa hii ni kwa mteja na mfanyaji kazi....wote mnategemeana.
Vyombo hivi pia vinapangwa, na kwa rangi, ili kuonekana mpangilio wake na kuvutia.
Ni vizuri kufanya hii project kwa uhakika na pasipo haraka sana...ili upate kitu kizuri, na tuwe wasikivu wa wataalam wetu wanavyotushauri. bila hivyo utakuwa unapoteza hela kwa kuto kusikiliza ushauri wa kuweka vitu vinavyodumu katika jiko lako....
Katibu kwa huduma hii hapa Homez Deco.