Wednesday, July 31, 2013

Moses busket Inauzwa.......


Imetumika miezi 2 tuuuuu bei ni 300,000/-

Wasiliana na 0657-417070 Sylvia. (ni wajina wangu)....

Ukarabati wa vyumba vyetu katika kipindi hiki cha kuelekea kusherehekea sikukuu.............

Tumeshazungumzia, sebule, dinning, korido, vyooni na sasa tunaelekea vyumbani na kisha tutakuja jikoni, na nje ya nyumba zetu.......

Katika eneo hili la chumbani, hapa ni mahali pa kupumzika, ama kulala unapohitaji, kama ni usiku ama mchana.......Mwili unahitaji kupumzika, na kama unahitaji kupumzika, basi hakuna budi chumba kiwe kisafi, kizuri, na kiwe na nafasi....

Hivi mi jamani hua ninashangaa kwakweli, kuona vyumba vimejaa vitu. na kama mnavyojua vyumba vyetu vya kulala hua ni standard size....kama ndio 12 by 12 ama 10 by 10....kama ni nyumba ya kupanga ama ni nyumba yako.......sasa kwanini mtu usiweke vitu ambavyo utavitumia, na kuliko kurundika vitu?

Kwa mfano, unakuta mtu kaweka kitanda 6 by 6, makabati , dressing table, shoe rack, stand ya pochi, na tv, kochi, hanger ya nguo etc......basi ni kurundika vitu tuuu

Cha msingi jamani kwanza angalia ukubwa wa chumba chako, na ikiwezekana ukipime kama hujui size yake....na baada ya hapo, weka vitu kulingana na ukubwa wa chumba......sasa utakuta chumba ni kidogo lakini mtu anaweka kitanda kikubwa ama kabati kubwa.....yote haya ni ya nini?

Na huko kwenye makabati kuna nguo nyingi mtu na zingine hazivaliki......yaani kabati mpaka linalemewa....sasa ukija kwenye viatu ni vingi mno, na vingine huvai labda kwa kuharibika, ama umevichoka....ila bado unavyo tuuuuu....

Naomba kushauri kua vitu ambavyo hutumii jamani GAWA......

Kwa kufanya hivi itakusaidia kupata nafasi na hewa izunguke katika chumba chako, kua na vitu vingi sio kupendezesha nyumba........

Kwani ukiweka vitu kulingana na chumba chako, tena kwa mpangilio kutakua na tatizo?

Kwa upande wa rangi za vyumbani, tafadhali rangi zipakwe zilizopoa, maana rangi nazo zinachangia kwa kiasi kikubwa mno katika kukufanya u relax.....

katika vyumba vyetu tukumbuke pia usafi wa kina, ukianzia usafi wa cyling board, madisha, mashuka...etc.....

Dressing table zetu jamani hua tunazisahau.......mafuta yakidondokea hua yanaacha alama, vitana navyo....etc

Rangi hizo baadhi ni.................
 Kama rangi ina kiza, basi ipakwe kwenye upande mmoja wa ukuta na  kuta zingine ziwe na rangi ambazo ziko angaavu...



Pazia nazo ni muhimu, katika vyumba vyetu, sebule, dinning, jikoni etc........

Kitanda ni utandikaji wako wewe mwenyewe, labda kiwe na mito mingi, ama mashuka 2 ama duvet etc....ni wewe tuu upendavyo,

Bila kusahau taa za chumbani, zisiwe na mwanga mkali mno.....waweza kuweka shades ili kupunguza mwanga, hii husaidia chumba kiongezeke mvuto zaidi pale itakavyofika usiku........

Thursday, July 18, 2013

Public Toilets and Bathrooms....

Umeshawahi kukutana na toilet ambapo ukipita kwenye korido, unasikia harufu mbaya inatoka na kusambaa korido nzima, ama kama tena na hiyo toilet iko karibu na sitting room ama dining room basi ndio harufu yote inasambaa................

Kumekua na tabia kwa asilimia kubwa, watu kudharau ama kuona kinyaa kufanya usafi kwenye vyoo....vya nyumba zao...ama kumuachia tuu msichana wa kazi afanye usafi ajuavyo bila kumfuatilia usafi umefanyika vizuri tena kwa dawa zinazotakiwa kutumika, maana utakuta ukuta una ukungu ama kutu , masinki nayo basi vurugu tuuuuuu.......


Baadhi ya toilets/bathrooms.....na asilimia kubwa yakwetu hua hatuweki hizi glass ambazo hua zinazuia maji kurukia kwenye toilets seats...




Asilimia kubwa ya huku kwetu siku hizi hua tunaweka tiles ukuta mzima wa toilet zetu, kitu ambacho ni kizuri na kinapendeza...pale tuu kama hizi tiles zime mechishwa vizuri kwa wale wanaoweka tiles za urembo. Kwa wale wanaoweka tiles za rangi moja nyeupe pia hupendeza..

Tatizo linakuja kwenye usafi. je usafi unafanyika mpaka kule juu, ama ndio unafanya usafi pale unapofikia tuu....

Maana kwenye kuoga lazima maji yatarukia ukutani, na kuacha madoa madoa ya uchafu. Jamani hua inaleta kinyaa pale unapoingia na kutaka kuoga ama kufanya shughuli zako zingine halafu unakuta toilet ni kuchafu...halafu ukizingatia ni  nyumbani kwako.......maana siku hizi hata vyoo vya kulipia ni visafi muda woteee.

Nina mshukuru sana MAMA  yangu kwakua alinifundisha usafi tokea mapema...kuna msemo usemao, mkunje samaki angali mbichi......

Professional ya Mama yangu ni Housekeer, na ana experience ya 17- 18yrs ya hotel na sasa ni mwalimu wa Housekeeping & Laundry katika chuo cha Taifa....u can emagine inakuaje nyumbani.....

Yaani ilikua ukiingia tuu toilet, haijalishi unafanya nini, ni lazima uhakikishe unaacha toilet safi, na kavu muda wote. Ukiwa unakwenda kuoga, basi hakikisha ukitoka ukuta ni mkavu, na chini kukavu, na sink la toilet ni kavu muda wote....

Na ile tabia ya unaingia kuoga, unalowesha, towels, ama toilet paper, alikua haipendi.... yaani akikuangalia tuu, unajua kasema nini...maana saa ingine alikua haongei anakutizama, mwenyewe unarekebisha kosa lako.......

Tena hata kama hauingii kuoga ama etc....toilets/bathroom zinachekiwa muda wote........sio eti mpaka uwende haja......

Ilikua hakuna cha msichana wa kazi ama mtoto wake...wote mnafanya kazi kama kawaida hakuna kuleana kizembe....maana mwisho wa siku na mtoto unakuja kua na nyumba yako mama hatokuwepo.

Hii husaidia sana kua kusafi.

Maana kwa upande wa hotels, kuna wale wanaofanya usafi katika public areas, kama ume notice ama umeona, hua mara kwa mara wanaingia toilets na kuangalia usafi na maeneo yote ya reception, etc.....na ndio maana tunaona hotels muda wote ni kusafi.

Ukiweka utaratibu huu wa kila mara kuangalia kama vyoo nivisafi, na kila anaeingia anahakikisha amekuacha ni kusafi, na kwa upande wa kufanya usafi unafanya usafi mpaka  juu ya tiles...na kutumia products nzuri za usafi na kuua vijidudu, na kuweka maua yanayotoa harufu nzuri, ama sprays etc za kuleta harufu nzuri. Nakuhakikishia sehemu hii itakaa safi, na kukavu kila muda.

Baadhi ya products za usafi:

 Hizi ni baadhi ya products za usafi ninazozifahamu, na hazina kemikali, na matumizi yake ni wewe ndio unapanga maana una dikute wewe mwenyewe kulingana na matumizi yako...


Kwa mahitaji ya products hizi wasiliana na 0754-006977 anaitwa Tija........na atakupa maelezo zaidi.

Tuesday, July 16, 2013

KORIDO ZA NYUMBA ZETU....


Naomba leo tuangalie upande wa korido, baada ya kua tumeshaona sitting room, dinning room........

Katika eneo hili, kwa upande wa kuanzia usafi na rangi ni muhimu sana kuzingatia
Korido nyingi hua hakuna dirisha ama madirisha...hivyo kunakua na kiza cha aina flan hivi.......kulingana na ulivyojenga.

Hapa kuna nyumba aina mbili: kuna ambazo ni fupi na kuna ambazo ni ndefu (urefu kutoka juu mpaka chini).......ingawa wengi wetu tunajitahidi kujenga nyumba ndefu kulingana na maendeleo na mabadiliko ya kila kukicha.

Mtakubaliana nami kua kwenye korido zetu hua zinachafuka mno, maana utakuta mtu akipita mwingine kashika na mikono yake michafu, ama mwengine anashika tuuu basi ilimradi tabu tupu, na hivyo kufanya korido kuchafuka, na kama ndio haukua umepaka hizi rangi za wash 'n' ware ama silk maana rangi za aina hizi hua unaweza kusafisha na maji na uchafu ukapungua ama kuisha kulingana na uchafu wenyewe.

Kama unaona ukuta wako hauridhishi, basi waweza kupaka rangi, kwa kuuandaa ukuta wako. Mwite mtaalam, akupe hesabu ya rangi inaingia kiasi gani na gharama zake na aina ya rangi.......hivyo atauandaa ukuta kwa kupiga msasa, na kuziba mashimo kama yako, nashauri mtumie skimming plaster smoothover za dulux, halafu apake rangi iliyokusudiwa kama ni za Dulux etc.......

Rangi za korido ni light colors, ama rangi zenye mwangaza......Kumbuka katika eneo hili hakuna madirisha hivyo mwanga kupenya ni asilimia ndogo mno, ni nyumba chache zenye madirisha katika eneo hili.

Sasa unapopaka rangi zenye kiza, korido inakua ni ndogo, na giza na haitakua na mvuto wowote, hata kama kuna taa ambazo utaziwasha wakati wa usiku.......

Baadhi ya rangi za kupaka korido ni hizi, ingawa inategemea pia na sitting room na dinning room umepaka rangi gani......





Hizi pia unaweza ukahitaji ziwe light zaidi....na zikafaaa pia.....ama kama zilivyo.....

Mara nyingi hua ninashauri ukitumia mtaalam ina kua ni rahisi kukuhauri ni rangi ipi itapendeza kulingana na ukubwa ama udogo wa korido yako......

Ukipaka rangi yenye kiza kwenye korido yako, itafanya kua ni ndogo zaidi na yenye kiza........ona rangi hizi na uone jinsi zilivyo  dark halafu upake kwenye korido yako:


Tunakaribisha maswali, na tunatoa ushauri pia....Karibuni


Dawa Ya Mende....

hongera sana kwa kazi nzuri unayofanya. nina shida moja nahitaji msaada wako nyumbani kwangu kuna mende sana kila sehemu , kama unaweza kujua dawa nisaidie hili nilitatue hili tatizo.  nijibu kupitia blog yako.

asante sana
mimi-Anna 


Homez Deco tumepata email hii kutoka kwa mdau wangu na anaomba usahuri kama inavyosomeka.....Na napenda kumjibu hivi.....

Unachotakiwa kufanya ni kutafuta sababu ya mende kuwa katika nyumba yako, na sababu ni kati ya hizi, :
1. hauweki vitu kwa mpangilio
2. nguo ni nyingi na ziko katika malundo
3. hautumii products nzuri za usafi
4. uchafu uliokithiri
5. mabaki ya chakula hayatupwi sehemu husika na kwa usafi
6. usafi pia haufanyiki ipasavyo etc...
Hizi ni baadhi ya points ambazo ningependa uzifanyie kazi.....kuanzia nje mpaka ndani....na inahitajika uache kazi ufanye kazi, nikiwa nina maana kua ujitolee siku moja ufanye usafi wa nyumba nzima.......ikiwezekana utoe vitu nje vipigwe na jua kwa muda hata wa siku mbili ama tatu, na ndani ufanye fammigation pamoja na nje.....
Kabla ya kuingiza vitu ndani, hakikisha unachagua vitu unavyovihitaji, usivyo hitaji kama viko katika hali nzuri gawa, kama havifai basi tupa sehemu husika.......

This time ingiza ndani vitu utakavyotumia na upunguze mlundikano wa vitu.....na usafi uwe ni wa mara kwa mara, na kwasababu umefanya fammigation, ile ni sumu fanya usafi vizuri........

NB:
Hakikisha unahusisha na majirani katika fammigation maana ukifanya wewe mende watakimbilia kwa wenzio. dawa ikiisha nguvu mende wanarudi.......

Homez Deco tunakaribisha ushauri zaidi.....


Friday, July 12, 2013

UPAMBAJI WA ENEO LA KULA CHAKULA ( DINING AREA)

Leo tuingie upande wa dining area, katika chumba hiki wengi wetu katika nyumba hua kinaangaliana na sitting room, na kwa wachache hua wamekitenga yaani kinakua na ukuta hukioni.....

Tuanze na kwa hawa ambao dining inaonekana......katika ukipamba chumba hiki, angalia kwanza unahitaji kiweje yaani kiwe na mandhali gani, na kisha angalia ni nini na nini ni cha kuondoa. kama kimechakaa ama kimekwisha, ondoa ili uweze kupata nafasi nzuri kwa kuweza kudesign.

Kwa wale wenye dining room inayojitegemea unaweza paka rangi tofauti maana humu kunajitegemea......

Ingia mitandaoni, ama nunua magazines za home deco...angalia mipangilio iliyoko huko na mpaka rangi.....halafu ukisha jua ni nini unataka, viandike, na uanze kutafuta, sasa hapa waweza kuja kwa mtaalamu wa mambo ya decorations (Homez Deco) ama ukafanya mwenyewe.

Fanya window shopping kwanza, na uangalie pia na ukubwa wa dining area yako.....wengi wetu tuna eneo dogo lakini bila kujua ama wengine hawajali, wanaweka meza kubwa ya watu 6 wakati eneo ni lakuweka meza ya watu 4.....hili jamani tuwe makini katika hili....(Kufanya window shopping inakusaidia kufanya manunuzi ndani ya budget uliyopangilia)

Contemporary Dining Room by Denver Architects & Designers Ashley Campbell Interior Design






Tukishajua na kupata mpangilio mzuri.....sasa paka rangi yako, na hakikisha rangi iwe kwenye kundi ama isipishane sana na ile ya sitting room yetu, hii ni kwa dining area ambayo inaangaliana na sitting room...

Hakikisha pia kama unapaka rangi ambayo ina kiza basi paka ukuta mmoja na taa ziwe ni za kutosha, na pazia zisiwe na giza, hakikisha pia madirisha yako yanaingiza mwanga wa kutosha,  na kuta zingine ziwe zina rangi ambayo ina mwanga maana isije kuleta giza hata mchana.........kwa upande wa fanicha pia waweza kuchanganya zikawa na rangi mbili...maana tumezoe tuu kufananisha seti ya viti inakua ni moja tuuu kwa upande wa rangi......waweza kuweka carpet pia iendane.........ingawa sio lazima kuweka carpet.....
Contemporary Dining Room by Fort Lauderdale Architects & Designers tuthill architecture


Mara nyingi hua tunapendelea sisi wataalamu wa decoration, kuweka chandalier dining area, maana inaleta mvuto wa aina yake katika chumba hiki, na isishuke sana, kuna vipimo vya kuweka ili hata mtu mrefu akinyanyuka asijigonge.......Mara nyingi Dining hua hatutakiwi kuweka furniture nyingi ili kuonekane kumependeza.......kabati lako, ama console table na kioo chake ama picha kwa juu kama hutaki kioo,  meza yako ya chakula, carpet ukipenda, maua juu ya meza, taa ya chandalier, pazia zako. Naomba tuangalie mifano hii ya dining katika picha na uone kama kumejazana furnitures humu, na ndipo mtakapo kubaliana nami kua hata vitu vichache hupendeza pia......

Thursday, July 11, 2013

MITO YA SOFA ........


 karibuni, mito bado iko.................

TATIZO LA PANYA .........SWALI KUTOKA KWA MDAU WETU.....


Mambo Homez Deco. 

Ninaishi nyumba ya kupanga nasumbuliwa sana na panya. hata wakiisha ni kwa kipindi maana wapangaji wenzangu hawatilii umakini na wanatoboa sakafu na kuingia ndani hata ukiziba mashimo wanatoboa tena. Nisaidie nifanyaje.

From,
Angel.






Tumepokea email hii kutoka kwa mdau wetu, kama isomekavyo kua anasumbuliwa na tatizo la panya nyumbani, na ningependa kumjibu kama ifuatavyo......

Kwanza kabisa panya wanapenda mazingira ambayo ni machafu, na kama ndio mnakaa wengi, basi ukiwa unaweka wewe dawa wenzio hawaweki, unakua haujatibu tatizo la panya kabisa.......

Kinachotakiwa ni kua, wote mkubaliane kuweka dawa, na pia mfanye usafi wa mazingira kwa ujumla.....na mshirikiane katika hili, na usafi uwe ni wa ndani mpaka nje, na ndio muweke dawa, na muendelee na utaratibu huo mpaka panya wakiisha, na uwe ni utaratibu wenu wote wa kuweka dawa mara kwa mara na usafi uzingatiwe......


Tunakaribisha maoni katika hili kumsaidia dada Angel.......






MAPAMBO YA SEBULENI (SITTING ROOM) KATIKA MAANDALIZI YA SIKUKUU.....


Homez Deco imeona ni vema kuanza kuangalia chumba kimoja kimoja katika upande wa mapambo kwa kadri ya uwezo wa mtu mwenyewe.....

Kuna kama makundi matatu hivi kwa upande wa kupamba nyumba zao....
Kundi la kwanza ni jamii ya Waarabu:
Mtakubaliana nami kundi hili la kwanza wao hupenda sana nyumba zao, kwa mapambo na hua ni mara kwa mara huzipamba.......

Kundi la pili ni wale wote wanaopamba nyumba ikikaribia sikukuu:
Kundi hili la pili lenyewe ni mpaka sikukuu ikaribie ndio nyumba zipambwe, na ikisha sikukuu basi inasubiriwa ingine.....

Kundi la mwisho ni wale wanaopamba kwa msimu......
Hili la mwisho wao ni kwa msimu, yaweza kua ni kila baada ya miezi 3 ama miezi 6 ndio wanapamba nyumba zao......




Ila pia haijalishi wewe ni kundi gani, maana pia tunaangalia na mifuko inachangia na hulka ya mtu pia.

Zifuatazo ni baadhi ya dondoo za upambaji wa sitting room yako:

1. Ndugu mdau, unaweza ukaanza kuanza kwa kuangalia sitting room yako imekosa nini ama inahitaji kitu gani kabla hata ya kuanza kufanyia kazi.......je ukuta rangi yake inaridhisha, ama makochi yanahitaji kubadilishwa kitambaa au kusafishwa, ama kununuliwa mengine, ama pazia ziwe zingine, je sakafu yako iko nzuri, carpets, meza ya tv, taa, cyling board.etc

2. Baada ya kujua nini utahitaji kukifanya, unaweza kumtafuta mtaalamu wa kupamba nyumba ama  ndio uanze kuzunguka madukani, ama kwenye websites/blogs za mambo ya decorations za majumbani na uweze kujua vitu vipya vinavyokwenda na wakati, na kipi umekipenda na kujua pia bei za vitu hivyo....hii itakusaidia kupanga budget yako na urembe sitting room yako kwa budget.

3. Kama ulimuingiza mtaalam kazi itakua rahisi, na hutopata stress, maana pia atakushauri ni nini cha kufanya katika sitting room yako iweze kupendeza.

4. Nunua vifaa vinavyohitajika, kama uliamua kupaka rangi ya ukuta, ama kama uliamua kubadilisha kitambaa cha makochi, ama uliamua kushona pazia mpya, na hata kununua mapambo ya ndani kwako......

5. Ningependa kusisitiza kua, kama unavitu vya kupunguza ndani katika sitting room yako, kama vimechakaa, ama umevichoka, etc....huu ndio wakati wake, haina haja wala maana ya kuendelea kukaa na vitu usivyovitumia maana vinajaza sana sanaa. sitting room yako bila maana yoyote ile......

6. Na itakapo kua imefika muda wa kufanya marekebisho na kupamba...basi kazi ianze na utajikuta kua kazi inamalizika mapema, na bila kuumiza kichwa chako ama kukuchosha......

Mwisho, utasherehekea sikukuu yako ukiwa na amani, na sitting room yako ikiwa safi na nzuri ya kuvutia...

 Hizi ni baadhi tuu ya designs za sitting room......







Wednesday, July 10, 2013

MSIMU WA KUPAMBA NYUMBA ZETU KATIKA KIPINDI CHA SIKUKUUU


Habari nduge wadau wangu wote kwa ujumla.......

Napenda kuwaletea mada ya kupamba nyumba zetu katika kipindi cha sikukuu......Yaweza kua ni kupaka rangi nyumba yako, kubadilisha fanicha kwa ujumla, ama kubadilisha mapambo yako ya ndani, ama pia kufanya set up ya mpangilio wako wa fanicha za ndani.....

Katika kipindi hiki cha mfungo wa Ramadhani, ndio muda muafaka wa kufanya maandalizi kwa ajili ya sikukuu ya Idd....usisubirie dakika za majeruhi ndio uanze kuhangaika kupamba nyumba yako....

Ukianza mapema hata na wewe pia inakusaidia kwa njia moja ama ingine kwa upande wa mapambo unakua haikupi tabu.

Sasa basi unachotakiwa kufanya ni kuangalia nyumba yako imekosa kitu gani, ama inahitaji kitu gani ili iwe nzuri naya kuvutia, ili hata wageni watakapo kuja basi usipate aibu, ama hata wewe mwenyewe, pia upate kusherehekea vizuri na familia yako....

Yaweza kua ni rangi ya nyumba......anza kutafuta mtaalam sasa ili uweze kujua gharama, na ujipange mapema hiii.......ama mapazia pia.......etc...

Karibuni sana Homez Deco kwa mahitaji ya kupambiwa nyumba yako na ushauri pia......








SITE YA MBEZI BEACH.....



 Rangi yoyote utakayo kwa ajili ya kitanda chako ama furnitures zako, utaipata hapa Homez Deco....Kitanda hiki ni cha mtoto wa kike ana miaka 5, na alitaka pink.....

 Kitanda kikiwa kinasetiwa neti

 Na huku kikiwa kinaendelea kusetiwa........



Kwa mahitaji ya fanicha za chuma karibuni Homez Deco.....

SITE YA KUNDUCHI....


Design yoyote ile utakayo tunaweza kukutengenezea.......tulipeleka vitanda hivi:








SITE YA BUNJU.........

Homez Deco, tulipeleka vitanda site ya bunju.......


 Homez Deco tulitengeneza vitanda na neti zake.....na huu ndio muonekano baada ya kazi kuisha.....

 Vitanda vikiwa vimeshaunganishwa......napenda kuongelea tena kuhusu magodoro, godoro ni lolote lile.....vitanda hivi vya chuma vinakubali magodoro yoyote yale.....




 Nahapa chaga zikiwekwa, na magodoro. pamoja na kufungwa neti......


Karibuni sana Homez Deco kwa mahitaji ya vitanda vya chuma, neti na fanicha zote za chuma...........

Monday, July 8, 2013

KUPAMBA KITANDA KWA KUTUMIA MITO.......

 Mandhali ya chumba chako cha kulala ni wewe ndie unae amua kiweje, na kipendeze vipi......Hapa leo tutazungumzia jinsi ya kupamba kwa kutumia mito.....Katika upambaji wa aina hii kwanza kabisa hakuna kanuni ya uweke mito mingapi katika kitanda chako.....ni idadi unayoitaka wewe...kulingana na ukubwa wa kitanda chako.....Mashuka pia yanachangia kwa kiasi kikubwa mno kupendezesha chumba chako......

 Siku hizi mashuka asilimia kubwa yanauzwa yakiwa na foronya nne na kuendelea......sasa ni wewe tuu mwenyewe unataka kitanda chako kiweje.........mfano kwenye kitanda hiki kuna mito 8. na size ya kitanda hiki ni n5 by 6, ambapo shuka/duvet hili lina foronya mbili, nikiwa nina maana mashuka huja na foronya zinazofanana na mashuka ndio maana unaweza kujua kua lina foronya ngapi....

Sasa hizi foronya zingine unahitajika kua mtundu kidogo, ili uweze kuchanganyia.....mito ya nyuma ni off white, rangi hii huendana na rangi yoyote ile, mito mingine ndio hii rangi ya mbele ambayo maroon, na ukiangalia kwenye shuka iko foronya hizi huja na mashuka uliyonunua, na ile rangi ya off white imejirudia tena... na mto wa mwisho umejirudia kwa rangi ya maroon na ua la off white.....na imependeza....kwa muendelezo huu sio lazima ukanunua kila kitu sehemu moja, nikiwa na maana sio sehemu nyingi wanakua na foronya za ku mechishia...waweza tembea tembea na kuulizia na kupata maduka ambapo utapata foronya hizo za ku mechishia....
Kwenye vitanda vyetu hivi hivi pia ukweka bed runner, hupendeza mno.....yaweza kua ni rangi zinazoendana ama zinazokaribiana  angalau,.......mfano ni huu hapa kua, kuna bed runner ya chui chui, halafu ikawekwa ya maroon kwa juu yake......na muonekano unazidi kuvutiwa kwa kuongezewa mito kwenye kiti cha kuvalia viatu, ile chui chui imejirudia, halafu maroon, na brown ambayo imetoka kwenye rangi za chui chui....

Nahapa hata ingetumika papo pia ingependeza...maana unachukua rangi za kwenye mashuka yako ndio muongozo wako katika upambaji wa kitanda chako......

Namna hii nakuambia unapumzisha mwili wako vizuri baada ya mihangaiko siku nzima na kuamka ukiwa na nguvu tele na mawazo mapya kwa siku inayofuata....

Upambajio wa nyumba yako unaanza na wewe mwenyewe, na sio mtu wa nje....ukishaa amua ndio mtu wa nje anaweza kukusaidia....

Homez Deco tunakukaribisha kwa maswali, maoni, ushauri, na hata huduma zetu katika hili na mengineyo mengi....Karibuni....

NB:
Homez Deco tutakusaidia kwa kiasi kikubwa kukutafutia foronya za ziada kwa ajili ya kumechishia mashuka yako....wasiliana nasi: 0713 - 920565